TANGAZO
Naibu waziri wa Maji Amos Makala,anatarajia kuanza ziara ya kikazi hii leo Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara kwa ajili ya kukagua mradi wa maji wa MANAWASA.
Aidha taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa malaka hiyo ya maji safi na usafi wa mazingira Masasi-Nachingwea imeeeleza kuwa naibu waziri huyo atapokelewa hii leo majira ya saa 4:30 asubuhi katika eneo la kijiji cha Nangoo,Halmashauri ya wilaya ya Masasi na baadaye kuelekea kwenye eneo la chanzo cha maji hayo eneo la MBWINJI.
Mara baada ya kutoka kwenye chanzo cha maji Naibu waziri huyo ataelekea kwenye matanki ya kuhifadhia maji yaliyoko katika kijiji cha Maili Sita Halmashauri ya mji wa Masasi ili kujionea namna ya uzalishaji maji unavyofanyika.
Kisha ataelekea mtandi na baada atapata chakula cha mchana kabla ya kuelekea huko Chinongwe na baadae Chiumbati.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD