TANGAZO
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Watendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Masasi pamoja na Halmashauri ya mji wa Masasi wameaswa
kuacha utamaduni wa kutegemea zao la korosho pekee kama chanzo kikuu cha mapato
katika halmashauri hizo.
Hayo yalisemwa jana
na katibu tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter wakati anatoa mchango wake
kwenye kikao cha ushauri cha wilaya ya Masasi (DCC) kwenye ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi.
Alisema kutoakana na
mabadiliko ya hali ya hewa nchini iko siku uzalishaji9 wa zao la korosho
unaweza kushuka mazingira ambayo yanaweza kusababisha Halmashauri hizo
kushindwa kujiendesha kutokana na kukosekana kwa mapato yatokanayo na zao la
korosho.
Kwa mujibu wa katibu
tawala huyo alisema kuwa ni vyema wataalamu wa kilimo kutoka kwenye halmashauri
hizo wakaanza kutoa elimu sambamba na kusambaza mbegu za kisasa za zao la alizeti
kwa wakulima ili liwe mbadala wa zao la korosho ambalo kwa sasa linaonekana
kuwa na changamoto nyingi katika uzalishaji wake.
Aidha amewaagiza
wakurugenzi wa halmashauri hizo kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa mbegu za
mazao ikiwemo ufuta pamoja na choroko ili kupunguza pengo lililopo kwa sasa
pindi zao la korosho linapoyumba.
Alisema wilaya ya
Masasi ina maeneo ambayo yanazalisha zao la mahindi kwa wingi ikiwemo vijiji
vya Namajani, Namatutwe na Chiwale maeneo ambayo yanaweza kuwekewa mkazo yakawa
kanda maalumu ya uzalishaji wa zao la mahindi kama yalivyo maeneo mengine
nchini.
Akizungumzia kuhusu
zao la choroko pamoja na ufuta alisema ni vyema halmashauri hizo zikatafute
wafanyabiashara wakubwa ambao watanunua mazao hayo lengo likiwa ni kuongeza
mapato ya ndani kwa halmashauri hizo zinazounda wilaya ya Masasi.
Kuhusu kilimo cha
umwagiliaji katibu tawala huyo alisema baadhi ya vijiji vya wilaya ya Masasi vimepitiwa
na mto Ruvuma ambao kwa sasa hautumiki kwa katika kilimo cha umwagiliaji ambapo
amewaagiza wakurugenzi kuangalia upya namna ya kuanzisha kilimo cha umwagiliaji
kwa kutumia maji yam to Ruvuma.
“Ndugu zangu uko
tunakoelekea ziko dalili za kushuka kwa uzalishaji wa zao la korosho… hivyo
kabla hatujafika hatua hiyo ambayo ni dhahiri itapunguza kwa kiasi kikubwa
mapato ya ndani ya Halmashauri zetu, hivyo ni vyema tujielekeze katika kutafuta
mbadala wa zao la korosho”.alisema.
Alisema watendaji
wawe wabunifu katika kuzifanya halmashauri hizo ziwe na mapato ya makubwa ya ndani
kwa kupanua wigo wa mapato itakayosaidia kuboresha miundo mbinu ya halmashauri
hizo.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD