TANGAZO
Fatuma Maumba, Mtwara.
Wananchi mkoani Mtwara wametakiwa
kuwalea watoto wao kwenye malezi ya dini ya kiislamu ili waweze kujengeka kimaadili,
hatua itakayowawezesha kukubalika katika jamii ya watu waliostaarabika.
Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa
jimbo la Mtwara Mjini, Hasnain Murji, wakati wa mazungumzo yake na waumini wa
dini ya kiislamu eneo la Mmart Chuo cha kilimo Mtwara, ambapo pamoja na mambo
mengine amechangia shilingi laki tano na mifuko hamsini ya saruji kwa ajili ya
kuendeleza ujenzi wa madrasa ya watoto ambao kwa hivi sasa wanatumia darasa
ambalo halifai kusomea.
Alisema ni vizuri jamii ikatambua na
kuelewa umuhimu wa kuwalea watoto wao kwenye maadili mema ya dini ya kiislamu
ambayo yataweza kuwasaidia katika maisha yao ya baadae, kutokana siku hizi
wototo wengi wamekuwa wakikiuka maadili ya dini zao.
“Mimi nina imani kabisa kijana yeyote
yule ambaye amesoma kwenye madrasa ama amelelewa kwenye dini ni tofauti
sana na vijana wa kwetu ambao wako mitaani…Ndugu zangu tunapata shida sana na
vijana ambao hawajaelimishwa kidini.
“Lakini nawahakikishia Mtwara hii
vijana ambao waliokuwa na elimu na wasiokuwa na elimu wanaweza kuja kupata
hifadhi lakini mtu asiyekuwa na elimu hana nidhamu au wewe una elimu huna
nidhamu bado nafasi utakosa, kwa sababu wenzetu wanaotoka nje wataangalia
maadili kwanza kwa hiyo lazima tuwalee watoto wetu kwa kuzingatia maadili ya
dini ya kiislam,” alisema Murji.
Kwa upande wake Mwalimu wa Madrasa,
Hamadi Mbwana, alimshukuru Mbunge wa Mtwara, Hasnain Murji kwa msaada alioutoa
kwani utapunguza changamoto waliokuwa nazo wa ujenzi wa madrasa ya watoto.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD