TANGAZO
Gari la wagonjwa lililotolewa na Mama Salma Kikwete. |
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Mke wa Rais ambaye
pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya wanawake na maendeleo nchini (WAMA) Salma
Kikwete leo ametoa msaada wa gari moja ya wagonjwa katika hospitali ya
Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.
Msaada huo wa gari la
wagonjwa alioutoa ni kutoka kwenye mfuko wa taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na
shirika lisilo la kiserikali la Sayeed Corporation ikiwa ni utaratibu wake wa
kawaida katika kushughulikia mahitaji ya msingi ya akinamama na watoto hapa
nchini.
Akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo alisema kupatikana kwa gari hilo ni kielelezo tosha cha
upendo mkubwa walionao shirika la Sayeed Corporation kwa wananchi wa mji wa
Masasi kwa kuwa takwimu zinaonesha kuwa akinamama wajawazito hupoteza maisha
kutokana na kucheleweshwa kufika katika vituo vya huduma za uzazi.
“Niliamua kukabidhi
gari hili kwenye Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Masasi, baada ya kubaini
kuwa akinamama wengi wanahitaji huduma ya usafiri ili kuja katika hospitali
hiyo kwa wakati”.Alisema Salma.
Kwa mujibu wa
mwenyekiti huyo wa WAMA alisema Hospitali ya Mkomaindo ni miongoni mwa
hospitali kongwe nchini ambayo imekuwa ikishirikiana na hospitali zingine
zikiwemo hospitali za wilaya za Nachingwea,Lindi,Newala,Mtwara pamoja na nchi
jirani ya Msumbiji na kwamba kupatikana kwa gari hiyo kutasaidia kuleta
wagonjwa wanaotoka katika maeneo hayo.
Gari la Wagonjwa lililotolewa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa Hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi.
Alisema Taasisi ya
wanawake na Maendeleo (WAMA) ilianzishwa ikiwa na malengo ya kuboresha afya ya
uzazi ya mama na mtoto kwa kununua na kutoa misaada ya vifaa vya afya katika
hospitali mbalimbali nchini, kufanya kampeni ya kuzuia maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Aidha mikakati
mingine iliyowekwa na taasisi hiyo ni pamoja na kuendesha kampeni za kufanya
uchunguzi wa saratani ya matiti n ile ya mlango wa kizazi sambamba na kutoa
elimu kwa waandishi wa habari na wananchi kwa ujumla juu ya umuhimu wa afya ya
uzazi salama.
Alisema akinababa pia
wanapaswa kuwa karibu na wake zao kwa kuwafanyia maandalizi ya rasilimali fedha
kwa kuwa vifo vingi vya wanawake na watoto hutokana na wananchi wengi kushindwa
kuwapeleka hospitali kwa wakati akinamama wanaoshindwa kujifungua kwa njia ya
kawaida.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wananchi wa mji wa Masasi (Hawapo Pichani) kwenye viwanja vya Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Masasi.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha alimshukuru
mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete kwa kuwapa msaada huo wa gari ya wagonjwa
litakalotumika katika wilaya ya Masasi.
Alisema msaada huo
umekuja kwa wakati na kwamba utakuwa umeokoa vifo vingi vya wanawake wajawazito
na watoto vilivyokuwa vinatokea hapo awali kwa kucheleweshwa kufika kwenye
vituo vya afya pamoja na hospitali ya Mkomaindo kwa wakati.
Mwisho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Andrew Mtumusha akitoa shukrani zake kwa mwenyekiti wa Taasisi ya maendeleo ya wanawake (WAMA) mara baada ya kupokea msaada wa gari moja la wagonjwa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkomaindo Dkt.Albano Nditi akipeana mkono na mke wa Rais Mama Salma Kikwete baada ya kukabidhi taarifa ya Hospitali ya Mkomaindo.
Mama Salma Kikwete akiangalia ndani ya gari hiyo aliyoitoa kwa hospitali ya mkomaindo Masasi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi akiwa ameshika Funguo ya gari hilo la wagonjwa mara baada ya kukabidhiwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Pichani ni vifaa vilivyopo ndani ya Gari hilo la Wagonjwa
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa kwenye picha ya Pamoja na baadhi ya watumishi wa ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake (WAMA) Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni katika hospitali ya mkomaindo Masasi mara baada ya kuwasili hospitalini hapo.
Mama SALMA KIKWETE akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa kimila (MAMWENYE)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wananchi pamoja na wanafunzi waliojitokeza kumlaki alipowasili kwenye viwanja vya Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Masasi.
Mama Salma Kikwete akimuangalia mtoto katika wodi ya uzazi katika hospitali ya mkoamindo alipofanya ziara ya kuona wakinamama hao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha akipeana mkono na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kumkabidhi gari ya wagonjwa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD