TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
MTOTO mwenye umri wa
miaka 14 (Jina linahifadhiwa) mkazi wa Njenga- Ndanda Halmashauri ya wilaya ya
Masasi mkoani Mtwara amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la
kulawiti.
Mbele ya mwendesha
mashtaka Iddi Athumani alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mwishoni mwa
septemba, 2014 majira ya saa 11:30 jioni huko katika kijiji cha Njenga Ndanda Halmashauri
ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Athumani aliieleza Mahakama
kuwa mshtakiwa huyo kwa makusudi alimlawiti mtoto mwenzake wa miaka tisa (Jina
linahifadhiwa) anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Ndanda
Halmashauri ya wilaya ya Masasi.
Alidai kuwa upelelezi
umekamilika na unaonesha mshtakiwa alitenda kosa hilo ila kwa kuwa mshtakiwa ni
mtoto aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu ambapo aliomba kuwa mtoto huyo
apelekwe kwenye gereza la wafungwa la watoto.
Baada ya maelezo ya upande wa mashtaka hakimu wa
mahakama ya wilaya ya Masasi Halfani Ulaya aliridhika na maelezo yaliyotolewa na upande
huo na kumtia hatiani mshtakiwa huyo kwa
kumpa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela .
Aidha mahakama ilitoa
agizo kwa daktari wa wilaya kumfanyia vipimo vya afya mtoto huyo huku Ofisa
maendeleo ya jamii pamoja na wazazi wa mtoto huyo wakitakiwa kutoa taarifa za
maendeleo ya ukuaji wake kabla hajasafirishwa kuelekea mkoani Morogoro liliko
gereza la watoto.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD