TANGAZO
Jumla ya shilingi milioni 89
zimetumika kwenye mpango wa kunusuru Kaya maskini sana kupitia awamu ya tatu ya
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF III katika Halmashauri ya mji wa masasi
mkoani Mtwara huku wanufaika na mpango huo wakielezea furaha yao.
Hayo yalisemwa jana na mratibu wa Tasaf Halmashauri ya mji wa
Masasi Joram Msyangi wakati wa zoezi la ugawaji wa fedha kwenye kaya masikini
mjini humo ambapo amewataka wanufaika na mpango huo kutumia fedha wanazozipata
kwa malengo yaliyokusudiwa na yenye tija kwa ustawi wa jamii.
Alisema baadhi ya wanufaika wa mpango huo
wamekuwa wakitumia fedha hizo kwa matumizi yasiyo na maana ikiwemo ulevi kitu
ambacho kinakwenda kinyume na malengo ya mfuko wa maendeleo ya jamii ambayo
lengo lake ni kuzinusuru kaya masikini
kama ilivyokusudiwa na kwamba kufanya
kinyume na malendo ya mpango ziweze kuishi vizuri.
Alisema wanufaika wanapaswa kutambua
kuwa ruzuku hiyo wanayopewa na serikali inapaswa kutumika huo ni kukosa
shukrani kwa serikali ambayo ina nia ya kuboresha maisha ya wananchi wake.
Kwa
mujibu wa mratibu huyo alisema Halmashauri ya mji wa Masasi imekuwa ikitekeleza
miradi ya Tasaf kwa kiwango cha hali ya juu na kwamba wanatarajia kufikia
malengo yaliyowekwa na serikali ya kuhakikisha kuwa kila mtanzania anakuwa na
maisha bora kupitia ruzuku hizo pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wanufaika wa mpango huo Rukia Bakari(55),wa
kitongoji cha Kagera,Hadija Rashidi(40) pamoja na Maria Mrope (66) wote wa
kitongoji cha Wapiwapi B waliupongeza mpango huo ambao umekuwa ukiwasaidia kwa
kiasi kikubwa katika kujikimu na maisha yao.
Mwisho.
Baadhi ya wanufaika waliokuwa wakisubiri kulipwa Ruzuku zao
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD