TANGAZO
Na Hamisi Abdelehemani,
Nanyumbu.
MFUMO wa ununuzi wa zao
la korosho kwa kutumia fedha za mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha ikiwemo
Benki imeelezwa kuwa ni chanzo moja wapo cha uwepo wa mzigo wa madeni kwa vyama
vya ushirika vya msingi (AMCOS) katika mikoa ya Lindi na Mtwara jambo linalodaiwa
kuwagandamiza wakulima wa zao hilo.
Hayo yameelezwa juzi na
mwenyekiti wa Chama cha ushirika cha msingi Cha Masyalele(AMCOS)kilichopo wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara Ahmedi Hassani alipozungumza na wandishi wa
habari waliotembelea wilayani humo kuangalia mwenendo wa malipo ya tatu(BONUS)
ya zao hilo kwa wakulima mkoani hapa.
Alisema licha ya uchanga
wa Chama chao kuwa ni kipya kuanza kununua mazao mwaka 2014 baada ya kuanzishwa
rasmi Chama hicho kufuatia baadhi ya wanachama kujigawa kutoka katika Chama cha
Sengenya ambacho kipo katika kata yao ya Sengenya wamefanikiwa kuwalipa vizuri
wakulima malipo ya majaliwa kwakuwa hawakukopa mkopo benki.
“Sisi tumetumia mfumo wa
kukusanya mazao kwa wakulima na kupeleka kuuza kwenye mnada moja kwa moja njia
hii tumefanikiwa kuwalipa wakulima wetu viruzi bila mifarakano kama vyama
vingine …mikopo kwenye taasisi za fedha hasa mabenki ni mzigo wa madeni kwa
vyama vyetu vya msingi,”alisema Hassani
Alisema njia moja wapo
ambayo wao wameitumia na kufanikiwa kuweza kuwalipa wakulima bila ya kikwazo ni
kukusanya mazao ya wakulama kisha kuyapeleka kuuza moja kwa moja kwenye mnada
mkuu bila ya kupitia kwenye Chama kikuu cha ushirika mkoani Mtwara (MAMKU)
Hassani alisema katika
msimu huu wa zao la korosho walikusanya tani 306 na kilo zipatazo 705 na kwamba
katika mnada wa kwanza waliuza kwa sh.1600 na wapili waliuza kwa sh.1529 huku
malipo ya tatu wamewalipa wakulima sh.220 na kueleza kuwa mikoapo katika
taasisi za imekuwa na lipa kubwa kwa vyama vya msingi.
Akizungmuza kwa niaba ya
wakulima wenzake wilayani humo,Saidi Yahaya alisema sababu moja wapo
inayowagandamiza wakulima kutoweza kupata faida katika zao la korosho mkoani
humo ni mfumo mzima wa ununuzi pamoja na vyama vyao kukopa kwenye taasisi za
kifedha ambapo serikali pia inapaswa kuboresha mfumo wa ununuzi wa zao hilo
Alisema mfumo wa ukopaji
fedha kutoka kwenye taasisi za kifedha kama Mabenki kwa vyama vya msingi
inaviumiza vyama hivyo pamoja na wakulima wake na kwamba serikali iweke mfumo
mzuri wa ununuzi wa korosho ili kuweza kumnufaisha mkulima tofauti mfumo uliopo
sasa wa stakabadhi ghalani.
Aliongeza kuwa iwapo
mkulima angekuwa analipwa malipo yake kwa mkupuo badala ya kulipwa kwa awamu
kama ilivyo kwa sasa hali za wakulima zingebadilika hata thamani ya zao hilo
ingekrudi kama zamani.
Mwisho.
KOROSHO ZIKIWA MBICHI
KOROSHO ZIKIWA TAYARI KWA KULIWA
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD