TANGAZO
Mamlaka ya Maji Safi
na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) inatambua tatizo la
kutokuwepo kwa Maji katika eneo la wakazi wa Maendeleo chini kwa muda mrefu
sasa. Mamlaka ina nia nzuri ya kutoa huduma kwa wananchi wote wa mji wa Masasi
na maeneo jirani ili kuifanya Mamlaka hiyo iendelee kutoa huduma bora kwa
wakazi wa mji wa Masasi.
Tatizo la kutokuwepo
kwa maji katika eneo hilo ni kutokana na “UCHELEWESHWAJI
WA RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU” kunakopelekea Mamlaka kukosa “MABOMBA” ya kuweza kuwaunganishia huduma ya maji
wakazi wa eneo hilo.
Hivyo, MANAWASA inatoa “WITO”
kwa wakazi wa eneo hilo walio tayari waweze kuchangia ununuzi wa Mabomba ya
maji ambayo huuzwa kwa kiasi cha shilingi 600,000/=
hadi 800,000/= kwa moja ili huduma hiyo
ipatikane na Mamlaka itachangia kwa kuleta wataalamu wa kuunganisha huduma
hiyo.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi wa MANAWASA Nuntufye David Mwamsojo (Pichani) amewataka wananchi wa eneo hilo
kufika ofisini kweke wakati wowote kwa ajili ya kuja kupata ufafanuzi wa namna
mtakavyotatua tatizo hilo.
Ahsanteni
Sana,
Naomba kuwasilisha.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD