TANGAZO
"mbele yako ni Tank la kuhifadhia maji hapa katika eneo la CHIUMBATI" Ni maneno ya Nuntufye David Mwamsojo Mkurugenzi wa MANAWASA akimwambia Naibu waziri wa Maji Amos Makala.Kulia kwa naibu waziri wa maji ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Pololet Kamando Mgema.
Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Chinongwe Wilayani Ruangwa ambapo amewahaidi kumaliza tatizo lao la madai ya fidia.
Mkuu wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) wakati wa ziara yake wilayani Masasi.
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) Nuntufye David Mwamsojo akisoma taarifa fupi ya MANAWASA kwa Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bernald Nduta akiteta Jambo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Kazumari Malilo(Simba wa Yuda) nje ya ofisi ya chama hiko.Mwenye Miwani ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Ramadhani Pole.
Naibu Waziri wa Maji AMOSI MAKALA(Katikati) akiwa nje ya ofisi za MANAWASA mjini Masasi kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bernald Nduta na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Masasi ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyasa (CCM) Andrew Mtumusha.
Naibu Waziri wa Maji AMOSI MAKALA akiteta Jambo na Mkurugenzi wa MANAWASA Nuntufye D.Mwamsojo nje ya Ofisi hizo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji Nchini.
Mkurugenzi wa MANAWASA Nuntufye David Mwamsojo mwenye kitabu mkononi akimpa maelekezo Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala wakati wa ziara yake na hapa ni katika eneo la kijiji cha CHIUMBATI wilayani Nachingwea.
Mkurugenzi wa MANAWASA akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji juu ya Mashine ya kusafishia Maji.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Pololet Kamando Mgema akimwongoza Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala kutembelea na kukagua mradi wa maji wa MANAWASA katika kijiji cha Chiumbati Wilayani Nachingwea.
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Salvius Kilowoko akiongea na wananchi wa kijiji cha Chinongwe wilayani Humo waliojitokeza kumsikiliza Naibu waziri wa Maji Amosi Makala
Wananchi wa Kijiji Cha Chinongwe wakiwa kwenye mkutano uliohutubiwa na Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala
Wananchi wa Kijiji cha Chinongwe wakimsikikiliza Naibu waziri wa Maji Amosi Makala.
Naibu Waziri wa Maji Amosi Makala akiwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Pololet Kamando Mgema alipomtembelea Ofisini kwake.
Naibu waziri wa Maji Amosi Makala,Msaidizi wake Pamoja na Mkurugenzi wa MANAWASA Nuntufye David Mwamsojo wakifurahia jambo katika eneo la kijiji cha Chiumbati wilayani Nachingwea.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD