TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Benki ya damu salama kanda ya kusini imefanikiwa kukusanya wastani
wa chupa za damu zipatazo 289 kupitia wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani lengo ni kuokoa maisha ya akina mama wanaojifungua na watoto waliochini
ya umri wa miaka mitano.
Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Mtwara Tabitha kirangi aliyasema
hayo jana alipokuwa akisoma taarifa fupi ya maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani ambapo mkoani humo sherehe hizo kimkoa zilifanyika katika viwanja vya
mashujaa vilivyopo katika manispaa ya Mtwara mikindani.
Alisema Benki ya damu salama kanda ya kusini iliendesha zoezi hilo
la uchangiaji wa damu katika Manispaa ya Mtwara pekee yake kupitia wiki hiyo ya
siku ya wanawake duniani na kwamba litaendelea katika Halmashauri zilizosalia.
Kirangi aliongeza kwamba kwa hatua inayofuata ya zoezi hilo la
uchangiaji wa damu salama katika Halmashauri zilizobaki ni kwamba utaratibu na
ratiba ya kuanza kuendesha zoezi la upimaji itatolewa.
Alisema wananchi wote wanapaswa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya
kuchangia damu pindi muda huo utakapo fika lengo kuu la uchangiaji huo ni
kuokoa maisha ya akina mama wanaojfungua na watoto waliochini ya umri wa miaka
mitano.
“Nitoe wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika hatua
inayofuata ya uchangiaji wa damu ili kwa pamoja tuweza kuoakoa maisha ya akina
mama wanaojifungua na hawa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano,”alisema
Kirangi
Aidha kirangi alisema kuwa kuhusu bima ya afya kwa wazee na kwamba
kuhakikisha kuwa wazee wanapatiwa matibabu ya uhakika na kwamba kupitia
maadhimisho hayo Halmashauri za mkoa wa Mtwara zimefanya zoezi la utambuzi wa
wazee.
Alisema kupitia zoezi hilo la utambuzi hadi tarehe sita ya mwezi
Machi mwaka 2015 jumla ya wazee 27,298 ambapo kati yao wanawake ni 12,985 na
wanaume 12803 walitambuliwa kwenye zoezi hilo ambalo hadi sasa linaendelea
mkoani humo.
Kirangi alieleza kuwa Halmashauri za Mtwara
Mikindani,Tandahimba,Mtwara na Masasi zipo katika hatua ya pili ya kuwakatia
wazee bima ya afya vilevile kupitia maadhimisho hayo mkuu wa mkoa Dendego
ambaye ndiye mgeni rasmi katika sherehe hizo atakabidhi kadi za bima ya afya
kwa niaba ya wazee wote wa mkoa huo.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD