TANGAZO
Mkuu wa wilaya ya
Masasi mkoani Mtwara,Bernald Nduta amewaomba watendaji pamoja na viongozi wa
chama na serikali wa Halmashauri zote mbili zinazounda wilaya ya masasi kumpa
ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya Masasi (DCC) kilichoketi kwa
ajili ya kujadili mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo moja wapo likiwa ni
kuangalia na kufanya marekebisho katika mapendekezo ya rasimu za mpango wa
bajeti kwa Halmashauri zote mbili kwa mwaka wa fedha wa 2015/16.
Alisema katika kutekeleza
majukumu yake viongozi wa dini na wale
wa kimila wana nafasi ya kutoa mawazo yao pale wanapodhani kuwa panastahili
lengo likiwa ni kuifanya wilaya ya Masasi kubaki kileleni kwa mafanikio
mbalimbali.
Kwa mujibu wa mkuu
huyo wa wilaya ya Masasi alisema wilaya ya Masasi ni miongoni mwa wilaya ambazo
wakuu wengi wa wilaya waliopita wamekuwa na mafanikio makubwa katika uongozi na
kwamba hata yeye anahitaji atoke Masasi akiwa na sifa zitakazomwezesha kuwa
kiongozi wa juu nchini.
Alisema katika
utendaji kazi kwenye Halmashauri yoyote nchini ni lazima kuwe na ushirikiano
miongoni mwa watendaji, madiwani,viongozi wa vyama vya siasa,viongozi wa dini
pamoja na viongozi wa kimila na kwamba bila ushirikiano itakuwa ni kujidanganya.
“Mimi ni kiongozi
kama viongzoi wengine…kuwa mkuu wa wilaya hainifanyi kuwa tofauti na wananchi
waliokiweka chama tawala madarakani,ni kweli kuwa wapo baadhi ya viongozi
wakipata madaraka hudharau watu,hushindwa kusalimia lakini mimi nahaidi mbele
yenu kuwa siko hivyo na karibuni ofisini kwangu”.alisema Nduta.
Alisema nitahakikisha
kuwa nafanya maamuzi kwa kuzingatia misingi na kanuni zilizowekwa bila kubagua
mtu yoyote na kwamba iko haja pia kwa watendaji wa halmashauri zetu mbili
kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumzia kuhusu
daftari la kudumu la wapiga kura,alisema ziko taarifa kuwa wapo baadhi ya watu
wanaowashiwishi wananchi wasijitokeze kwenda kujiandikisha kwenye daftari la
kudumu la wapiga kura kwa madai kuwa wakati wa uchaguzi watatumia vitambulisho
vyao vya awali.
Kuhusu elimu,Nduta
amewaagiza maofisa watendaji wa kata na vijiji kufanya msako wa nyumba kwa nyumba
kuwabaini watoto wote ambao hawajaripoti shuleni hadi sasa na atakayeshindwa
kutimiza jukumu lake basi atafute shughuli mbadala ya kufanya.
Pia amewaagiza
wakurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi pamoja na Halmashauri ya wilaya ya
Masasi kuhakikisha kuwa wanakamilisha ujenzi wa maabara ifikapo machi 30 mwaka
huu ili kuendana na agizo alilolitoa mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego
wakati wa ziara yake wilayani humo ilizozitaka halmashauri zote kukamilisha
ujenzi huo.
Mwisho.
MKUU wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta akisalimiana na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Eng:Silaji Mbuta wakati anawasili kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya Masasi hii leo. Kushoto kwake ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Juma Satma
Mkuu wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta akipeana mikono na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM Ramadhani Pole mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ya Masasi hii leo katika ukumbi wa Miduleni.
Mheshimiwa Bernald Nduta mkuu wa wilaya ya Masasi akitoa ufafanuzi wa jambo kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Masasi Kazumari Malilo (simba wa yuda-mwenye Balagashia) mbele yake ni katibu tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD