TANGAZO
UTANGULIZI:
Katika ahadi zangu
wakati nagombea sijawahi kuahidi mashine za kusaga. Kama wana shida ya mashine
za kusaga waseme wasaidiwe.
1. Ernest Wendeleni, Chikunja.
Hakuna
zahanati Chikunja, uliahidi utajenga mpaka leo kimya. ?
Jibu:
Kwanza niseme kuwa Ernest hajafika Chikunja kwa zaidi ya miaka mitano. Chikunja
kuna zahanati inafanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano sasa na wananchi wanapata
huduma. Hata hivyo tutaendelea kuhakikisha huduma za afya zinakuwepo na
zinapatikana kama ilivyopangwa.
2. Hassan Hassan Misinzo, Ndanda.
Uliahidi
utahakikisha kuna mashine za kusaga mpaka sasa hakuna. Kwa nini hukutimiza
ahadi hiyo?
Jibu:
Katika ahadi zangu wakati nagombea sijawahi kuahidi mashine za kusaga. Kama
wana shida ya mashine za kusaga waseme wasaidiwe.
3. Hassan Mpalanga. Masasi Mjini.
Hakuna vituo maalumu vya usafiri katika maeneo mengi, lini
utabadilisha mandhari ya mji wa Masasi iwe ya kupendeza?
Jibu:Tuna
stendi kuu ya mabasi Masasi mjini, ambayo ina kituo kikubwa cha mabasi ya
mikoani na ya ndani. Hata hivyo tumeshatengeneza eneo la kujenga stendi kubwa
kwa sababu kuna ongezeko kubwa la watu na maendeleo. Eneo hilo lipo karibu na
uwanja wa ndege.
4. Prisca Mlaponi, Nagaga.
Hospitali ya Mkomaindo bado inakabiliwa na uhaba wa dawa na
vitanda. Uliahidi tatizo hilo litakwisha. Vipi mpaka sasa unatusaidiaje?
Jibu:
Ni kweli kulikuwa na uhaba wa vitanda na dawa, nilitafuta wafadhili, nikapeleka
vitanda na magodoro. Magodoro ya ‘ICU’ yalinunuliwa ili kusaidia wagonjwa
mahututi lakini ieleweke kuwa suala la dawa ni tatizo la nchi nzima.
Nimejitahidi kufanya vikao na halmashauri ili kuhakikisha kuwa fedha zinazopatikana
zinunue dawa muhimu. Nilimueleza Rais kuhusu tatizo hili, alitoa muongozo
kutatua hilo. Sisi viongozi tunalifanyia kazi bado.
5.Deniss Chimwaga, Liwale
Kwa nini umeme mpaka sasa haujafika katika maeneo mengi. Huoni
kuwa uchumi wa Masasi utaimarika kama umeme utakuwepo?
Jibu:
Nilipoingia madarakani, umeme ulikuwepo katika maeneo ya mijini tu. Lakini kwa
kipindi nilichokaa madarakani umeme umeendelea kuwepo katika maeneo mengi kwa
kupitia wakala wa umeme vijijini, REA. Hata hivyo umeme utaingia vijijini hatua
kwa hatua, umeme utawekwa kama nilivyoahidi. Alipokuja Rais Jakaya Kikwete na
Nape Nnauye, nilitoa wazo, kuwepo kwa programu maalumu ya kusambaza umeme
vijijini, wananchi watashindwa kuelewa kuwa gesi imewanufaishaje. Niliomba pia
katika ilani ya CCM, Masasi ipewe kipaumbele kupata umeme.
6. Christopher Saimon Mtambalike, Chigugu.
Ufaulu ni mdogo sana shule za Masasi, mimba za utotoni
zimekithiri na elimu ni duni kwa ujumla. Utaliondoaje tatizo hili?
Jibu;
Ni kweli kabisa. Sababu ya elimu duni ni kwanza changamoto kutoka kwa wazazi
kutowaandaa watoto kielimu. wapo tayari kuwasomesha watoto hadi darasa la saba
tu, baada ya hapo hawataki. Kuna shule za kata maeneo mengine kuna shule mbili
lakini wazazi wanakataa kuwapeleka watoto. hawafanyi mandalizi mazuri kwa
watoto. Lakini pia kuna upungufu wa walimu suala ambalo nimelipeleka wizarani
na wananisaidia. Kuna upungufu wa madarasa lakini fedha za mfuko wa jimbo
zimesaidia. Wazazi wapo tayari kuchangia harusi, unyago wa kifahari lakini
kupeleka watoto shule wanakuwa wagumu. Viongozi wanahamasisha na kujenga shule
za sekondari, msingi na vyuo lakini bado kuna tatizo kwa wazazi.
7. Alfred Mitande, Liwale.
Wanafunzi wengi wanatumikishwa kazi wakiwa shuleni hali
inayosababisha washindwe kufanya vizuri kwenye masomo. Je, utatusaidaje kuondoa
tatizo hili.
Jibu:
Hata sisi zamani tulikuwa tunafanya kazi shuleni na elimu ilikuwa juu. wazazi
wa sasa hawataki watoto wafanye kazi. leo hii ni shule chache zenye mashamba.
Zamani ilikuwa tunalima shamba la shule halafu tunapata chakula shuleni hapo
hapo. Ninatembelea shule na kufanya vikao hilo ni tatizo ni dogo sana. lakini
kwa sasa wazazi hawataki hilo, wamebadilika hivi kweli mwalimu atashindwa
kumtuma mwanafunzi ndoo ya maji. Kazi nyingine ni sehemu ya wajibu wao.
8. Anna Martin, Chikunja.
Uliahidi visima katika vijiji vyote vya masasi na kuwa tatizo la
maji litapungua. Vipi mpaka leo hakuna matokeo chanya.
Jibu;
Nilipoingia madarakani kulikuwa na shida ya maji kuanzia mijini hadi vijijini.
Ndoa zilikuwa mashakani, lakini hilo tatizo limepungua kwa kiasi kikubwa. Nina
mradi wa maji Liwale ukikamilika utasaidia vijiji vitatu ambavyo ni Lilala,
Muungano na Nanyindwa. Kuna mradi upo tayari kijiji cha Mtakuja wananchi
wanapata maji. Kuna mradi Nambawala Nanganga, Ndanda, Chipute na Nkwera kote
miradi inaendelea kuwasaidia wananchi wapate maji. Mradi ukikamilika utahudumia
vijiji hivyo. Kuna miradi ya mabwawa huko Muungano na Chiwale. Hizo zote ni
jitihada kuhakikisha jimbo langu linapata maji.
9.Happiness Namulimuka, Liwale.
Usafiri wa bodaboda unatumika kufanya matukio mengi ya uhalifu
wilayani Masasi, je, utalitatuaje hili?
JIBU:
Bodaboda zinawasaidia wananchi kuanzia mjini na vijijini, kama zinatumika
katika uhalifu, hilo suala ni la kiusalama zaidi. Sijawahi kupokea malalamiko
hayo kwangu na kama wanapeleka malalamiko polisi basi wanapeleka sehemu sahihi.
Hata hivyo nitazungumza na mkuu wa mkoa na kupata ukweli, kama ni kweli
zitafanyika jitihada za kuondoa tatizo.
10. Victor Kasembe, Masasi Mjini.
Hatukusikii mara kwa mara bungeni ukiwatetea wananchi wako kama
wabunge wengine. Je, tutakupaje kura kwa msimu huu?
Jibu;
Nafikiri Victor husikilizi kipindi wala hufuatilii. Ninayo orodha ya maswali
ninayouliza bungeni. Zipo rejea za maswali na michango yangu na nina orodha ya
kila kitu ninachofanya bungeni. Sikurupuki kuzungumza mambo ambayo si ya
msingi. Maendeleo haya yote nimeyapata kupitia michango yangu na maswali
ninayoyatoa bungeni. Victor nakuomba unipe kura yako ili niendelee
kuzishughulikia kero nyingine zilizopo Masasi.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD