TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia, amewata
wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule ambao walibahatika kuchaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hii Waziri huyo, alisema wazazi wanatakiwa kuwapeleka watoto wao shule
kwani elimu ndio itakayosaidia waweze kunufaika na uchumi wa gesi ambao unakuja
katika mkoa wa Mtwara.
“Niwaombe tu wazazi wenzangu wawapeleke watoto
wetu katika shule na wahakikishe waliochaguliwa wote wanaenda kidato cha kwanza
na tusomeshe watoto kwa sababu elimu ndio itakayotusaidia tuweze kunufaika na
uchumi wa gesi ambao unakuja katika mkoa wetu wa Mtwara bila kusomesha watu
tutabaki kulalamika hata kama viwanda vitajengwa kwa mamia,” alisema Waziri
Ghasia.
Alisema Kama
watoto wa mikoa ya kusini hawatapata elimu basi wataishia kufanya kazi za
chini sana ambazo hazina hadhi hivyo watashindwa kunufaika ambapo amewaomba
wazazi kutilia mkazo suala la elimu kwa watoto wao.
“Ndugu zangu
bila kujibana na kujinyima watoto wetu hawatasoma kwani wote sisi hapa
tunaozungumza tulikuwa ni watoto wa wazazi wa kawaida sana lakini walijibana
wakatusomesha na sasa hivi wanayaona matunda”. Alisema Ghasia.
Hata hivyo
Waziri Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini ameipongeza wilaya yake
ya Mtwara Vijijini kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka
jana ila amewata wasibweteke na matokeo mazuri waliyoyapata na badala yake
wakaze buti ili waweze kushika nafasi ya kumi ama ya tatu kitaifa.
“Naomba niipongeze wilaya yangu ambayo
imeshika nafasi ya pili na pia niupongeze Mkoa kwa ujumla kwa sababu mwaka 2013
mkoa wa Mtwara katika matokeo ya kidato cha nne tulikuwa wa tatu kutoka mwisho
lakini mwaka 2014 tumekuwa wa kumi kitaifa…kwa hiyo kwa kweli tumesonga mbele
sana lakini hata hivyo pamoja na pongezi hizi tusibweteke bado tuna kazi kubwa
sana ya kufanya ili tuweze kufanya vizuri tena.
Waziri Ghasia,
alisema siri ya mafanikio ya kufanya vizuri mwaka 2014 Kama alivyosema kwamba
mkoa wa Mtwara kwa sababu walikuwa wa tatu kutoka mwisho Waziri Mkuu Mizengo
Pinda, aliomba apate maelezo, kwa nini wameshika hiyo nafasi ya tatu kutoka
mwisho na ajue mikakati yao ikoje ili kuhakikisha wanasonga mbele.
Kwa hiyo kama mkoa ilibidi utoe maelezo lakini
huwezi kupeleka mikakati alafu usiitekeleze kwa hiyo walijiwekea mikakati na
waliitekeleza na mwisho wa siku wakafanikiwa kushika kumi bora Kitaifa mwaka
jana, lakini kitu kingine pia ni ushirikiano na kuthamini walimu katika maeneo
yao.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD