TANGAZO
Na FATUMA MAUMBA,MTWARA.
MKUU wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amewataka wanawake wajasiriamali mkoani huo, kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya mashujaa kupeleka bidhaa zao ili waweze kujitangaza kwenye wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Dendego ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuongeza kwamba, lengo la maadhimisho hayo ni kutoa taarifa hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali na asasi mbalimbali katika kumwendeleza mwanamke kiuchumi na kijamii.
Hata hivyo Dendego, amesema kwamba malengo mengine ni pamoja na kuendelea kusisitiza umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika shughuli za maendeleo kwenye ngazi zote ili kuharakisha mabadiliko chanya yanatoke katika jamii.
Pamoja na mambo mengine Dendego amezungumzia suala la mauaji ya albino na kukemea vitendo hivyo visiendelee tena.
“Kama mama, kama mwanamke na kama kiongozi kwa kweli narahani sana haya mauaji ya albino yanatia uchungu sana na kweli inatia haibu kwa Taifa letu hata kama inatokea Kahama lakini bado ni Tanzania katika karne hii bado watanzania tumekuwa na imani potovu ya kutumia viungo vya binadamu kwa ajili ya kujipatia utajiri kwa hiyo katika maadhimisha siku wanawake duniani lazima tutasema na lazima tutapaza sauti zetu ili watusikie wenzetu” alisema Dendego na kuongeza:
“Kwanza haya mambo kwa kiwango kikubwa yanafanywa na watoto wa kiume kwa kweli wanatuumiza sana sisi wanawake,na hatua tuliofikia sasa mpaka kwenda kumnyanganya mama mtoto mgongoni alafu uende ukamkate ukimuua huku akiona kwa kweli tumefikia hatua mbaya sana ni vizuri tuhakikisha ukimuona mtoto wa mwenzio uonekane umemuona mtoto wa kwako.
Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Uongozi wa mkoa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mkoani na wilayani, wamepanga kufanya shughuli mbalimbali kama vile kuchangia damu kwa ajili ya Hospitali ya Rufaa ya Ligula na vituo vya kutolewa huduma ya afya, kufanya usafi wa mazingira maeneo ya umma, upimajiwa saratani ya mlango wa uzazi, matiti pamoja na upimaji wa VVU.
Mwisho.
MKUU wa mkoa wa Mtwara Halima Omari Dendego wakati anaongea na waandishi wa Habari hii leo ofisini kwake.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD