TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
Jamii imeaswa kuwahimiza wanafunzi kusoma vitabu kwa lengo la kuongeza ujuzi na maarifa kwa watoto hao kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo za sanaa na burudani.
Aidha serikali kwa kutumia mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo mradi wa Tz 21st pamoja na “BETTER NATION FOUNDATION” yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam yamekuwa yakiratibu zoezi la siku ya uhamasishaji usomaji vitabu katika kukuza stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wa shule za msingi nchini.
Pia shughuli zingine zinazofanywa na Better Nation Foundation ukuzaji na uboreshaji wa elimu ya msingi na kwamba zoezi hilo limeanzia Pemba na kwa sasa ni mkoani Mtwara ambapo matamasha mengi yaliyofanyika yameonekana kuzaa matunda.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya siku ya uhamasishaji kusoma iliyofanyika katika shule ya msingi Mumbaka, Halmashauri ya mji wa Masasi mkurugenzi wa taasisi ya Better Nation Hans Gabriel alisema taasisi yake imekuwa ikihamasisha jamii katika kusoma kwa kutumia sanaa za maigizo,kwaya ,ngonjera,ngoma pamoja na mashairi kwa lengo la kuifanya jamii kuwa mwamko wa kusoma vitabu.
Wapiga ngoma wa kikundi cha Better Nation Foundation wakifanya mambo yao hii leo katika viwanja vya shule za msingi Mumbaka Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.
WANAFUNZI wa shule ya msingi Mumbaka Halmashauri ya mji wa Masasi wakiimba kwaya wakati wa sherehe za uhamasishaji wa kusoma vitabu.
WANAFUNZI wa shule ya msingi MARIKA wakiimba kwaya
WAZAZI na walezi waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya kuhamasisha kusoma
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD