TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Mkuu wa
mkoa wa Mtwara Halima Dendego leo
amewaongoza maelfu ya akinamama mkoani Mtwara waliojitokeza kwa wingi huku
wakiwa na hamasa kubwa katika kilele cha
maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa
Mkoani humo.
Akizungumza
wakati wa sherehe hizo mkuu huyo wa mkoa wa Mtwara alisema wanawake nchini
waache kulalamika kuwa wananyanyaswa na wanaume na badala yake watumie fursa ya
elimu na uongozi waliyoipata hasa katika kipindi cha utawala wa awamu ya nne wa
Rais kikwete.
Alisema
ni ukweli usiopingika kuwa serikali kwa kushirikiana na asasi zisizo na
kiserikali zimekuwa na harakati mbalimbali zenye lengo la kumkomboa mwanamke na
kwamba kwa sasa hali ilivyo licha ya changamoto kadhaa kuwepo wanawake
wameendelea kupewa fursa mbalimbali za uongozi.
Alisema
changamoto kubwa inayowakabili wanawake ni kutopendana kwao hasa wakati wa
kugombea nyadhifa mbalimbali serikalini na kwamba kama hali hiyo ikiendelea
basi itakuwa ni ndoto za alinacha kwa wanawake kufikia malengo waliyojiwekea
ikiwemo uwiano sawa na wanaume wa 50/50.
Kwa
mujibu wa Dendego alisema elimu ndio chombo pekee kinachoweza kumkomboa
mwanamke na kwamba wakati sasa umefika kwa wazazi kuacha mara moja tabia ya
kutumikisha watoto wa kike majumbani huku wengine wakiozwa kwa wanaume wakiwa
na umri mdogo kwa kigezo kuwa kumpeleka shuleni mtoto wa kike ni kupoteza muda.
“Wazazi
suala la kutopeleka watoto wenu shuleni katika mkoa wa Mtwara iwe mwisho…na
sitaki kusikia wilaya yoyote iliyopo mkoani Mtwara ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi
wasioripoti shuleni na nawaagiza wakuu wa wilaya mkasimamie hilo”.alisema
Dendego.
Awali
akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Mtwara kuzungumza na wanawake hao, Mkuu wa wilaya
ya Mtwara Fatma Ally alisema wanawake wanapaswa kuwa wajasiliamali na waache
tabia ya kutegemea waume zao kwa kila kitu ambapo kwa kufanya hivyo ndiko
chanzo cha wao kunyanyaswa.
Alisema
wilaya ya Mtwara imejipanga kuendesha mafunzo ya ufugaji kuku wa kienyeji kwa
wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana na kuwa wategemezi
kwa kila kitu.
Mwisho.
MWANAMKE akionesha umahiri wake wa kuendesha Tractor katika viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Ni Bi Anjelina Stehano Mbesigwe kutoka Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara akionesha bidhaa zake kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani.
Wanawake pia wanaweza pichani ni mwanamke akiwa anaendesha Bajaj kwa umahiri kabisa alipokuwa akipita mbele ya mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika hii leo kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Mtwara.
Hiyo ni kazi ya wanawake pia kama unavyoona kwenye picha mwanamke huyo akifanya vitu vyake uwanja wa Mashujaa Mtwara.
Mkuu Mpya wa wilaya ya Mtwara FATMA ALLY aliyehamia hivi karibuni kutoka wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuzungumza na wanawake wa mkoa wa Mtwara.
MKUU wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiwaongoza wanawake kucheza nyimbo ya "MWANAMKE SIMAMA IMARA" tena kwa kukimbia mchakamchaka kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mtwara hii leo.
OFISA Maendeleo ya Jamii mkoa wa Mtwara Bi.Thabitha Kirangi akiongea wakati akisoma Hotuba yake kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
MWANAMKE Akiendesha Gari ya Zimamoto kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mtwara katika kuionesha jamii kuwa na wao pia wanaweza kufanya kazi kama wanazofanya wanaume.
Mwanamke mwingine akienndesha Gari ya Polisi Mkoa wa Mtwara
Kikundi Cha kwaya cha SAYUNI kikitumbuiza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siu ya wanawake duniani katika viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara.
Wanawake mkoani Mtwara wakiwa kwenye maandamano huku wakiwa wamebeba mabango maandamano yaliyoanzia kwenye maeneo ya Bima hadi viwanja vya mashujaa mjini Mtwara.
WANAFUNZI wa sekondari mbalimbali mkoani Mtwara nao hawakuwa nyuma wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani yaliyoadhimishwa kimkoa mkoani Mtwara.
MABANGO mbalimbali yaliyobebwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mama naye akionesha umahiri wake mbele ya mgeni rasmi kwa kupita akiwa anaendesha Baiskeli.
IDARA ya mahakama pia mkoa wa Mtwara ilileta wanawake waliopita mbele ya mkuu wa mkoa wa Mtwara wakiwa wanaendesha gari hiyo pichani.
KIKUNDI CHA KWAYA CHA SAYUNI...
MKUU wa mkoa wa Mtwara Halima Omari Dendego akicheza Segere na wanawake wa Mtwara....
Ni Burudani na shangwe ndizo zilizotawala kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mtwara wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Newala Kapteni George Huruma Mkuchika akimkabidhi kadi Bimkubwa SHARIFA YUSUPH kadi ya CHF zilizoandaliwa kwa ajili ambao wamepewa bure ili wapate huduma za matibabu bure.
BAADHI ya wazee waliopatiwa kadi za CHF
MABINGWA wa mchezo wa NETIBOLI Manispaa ya Mtwara Mikindani katika mashindano yaliyoandakiwa kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani wakifurahia mara baada ya kupewa kikombe chao cha ushindi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
BENKI ya CRDB mkoa wa Mtwara yakabidhi mapipa 20 ya takataka kwa nkuuu wa mkoa wa Mtwara wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD