TANGAZO
Benki ya CRDB mkoani Mtwara imetoa msaada wa mapipa ya huduma ya
takataka 20 yenye thamani ya sh.2.4 milioni kwa hospitali ya mkoa huo ya Ligula
kwa lengo la kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.
Msaada huo umetolewa jana kwa mkuu wa mkoa huo Halima Dendego
kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo kimkoa mkoani humo
sherehe hizo zilifanyika kwenye viwanja vya mashujaa mkoani hapa.
Akikabidhi msaada huo meneja utawala wa Benki hiyo mkoani
Mtwara,Amina Juma alisema Benki hiyo imeamua kutoa msaada huo wa mapipa 20 kwa
ajili ya kuboresha huduma ya afya katika hospitali hiyo ya Ligula na jamii kwa
ujumla.
Juma alisema afya ni jambo la msingi kwa binadamu hivyo katika
Benki ya CRDB kupitia kitengo cha huduma za kijamii imeamua kuangalia suala la
afya kwa jamii kwa kutoa msaada huo wa mapipa ambayo yatasaidia kukusanya
uchafu badala ya kutupa ovyo.
Alisema Benki hiyo imekuwa ikiwajali wateja wake kwa kuwapatia
huduma bora za kibenki na kwamba sehemu ya faida inayopatikana imekuwa ikitengwa
kwa kusaidia huduma za kijamii.
“Msaada huu wa mapipa 20 unalengo la kusaidia jamii kuhamasisha
jamii huduma ya utunzaji wa afya kwa kuweka safi mazingira yetu na kwamba
tutaendelea kutoa huduma kama hii mara kwa mara,’alisema Juma
Alisema Benki ya CRDB kila mwaka imekuwa ikitenga sehemu ya faida
yake kwa ajili ya kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,afya na
vikundi mbalimbali vya ujasiliamali kwa lengo la kuinua ustawi wa maisha kwa
jamii husika.
Akipokea msaada huo mkuu huyo wa mkoa Dendego aliishukuru Benki
hiyo kwa kutoa msaada huo wa mapipa 20 na kueleza kuwa umechangia suala la
uhamasishaji jamii kuhusu usafi wa mazingira.
Dendego alisema usafi wa mazingira kwa jamii ni suala ambalo
linapaswa kuwekewa mkazo hivyo CRDB imeonyesha mwanga kwa jamii juu ya umuhimu
wa utunzaji wa mazingira kwa kuweka safi mazingira ya mkoani hapa.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD