TANGAZO
Clarence
Chilumba,Masasi.
Baraza la madiwani Halmashauri ya mji wa
Masasi Mkoani Mtwara kwa pamoja limepitisha bajeti ya zaidi ya Shilingi Bilioni
18 zitakazokusanywa na kuelekezwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo kwenye kata na vijiji mbalimbali vya halmashauri hiyo kwa mwaka wa
fedha 2015/16.
Kati ya kiasi hicho cha fedha shilingi
Bilioni 1,850,000,000 inatarajiwa kupatikana kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato ya ndani
ambapo ruzuku kutoka Serikali kuu pamoja na misaada kutoka kwa wahisani
ikitarajiwa kuwa ni Shilingi Bilioni 17,374,522,738.
Aidha halmashauri inatarajia kutumia shilingi Bilioni 4,180,249,710 kwa ajili ya kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo kati ya hizo shilingi bilioni 110,000,000
huchangiwa kutoka kwenye vyanzo vya mapato vya Halmashauri ambayo ni sawa na
asilimia 60 ya makusanyo yake.
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango wa maendeleo na bajeti ya
halmashauri ya mji wa Masasi kwa mwaka
wa fedha 2015/16 katika kikao cha baraza
la madiwani wa Halmashauri hiyo
kilichoketi jana mkurugenzi wa
Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus
Kagoro alisema makadirio ya mwaka
2015/16 ni Shilingi Bilioni 18 na kwamba makadario hayo yamepanda kutoka
shilingi Billioni 14 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Alisema hadi kufikia Disemba 2014
halmashauri ya mji wa Masasi ilifanikiwa
kukusanya jumla ya shilingi milioni 607,494,290 sawa na asilimia 35 ya
makadirio yake ambapo kwa upande wa ruzuku hadi kufikia mwezi disemba 2014
shilingi milioni 5,660,892,723 sawa na asilimia 40 zilipatikana.
Kwa mujibu wa Fortunatus Kagoro alisema
licha ya kupitisha makisio ya bajeti ya
mwaka wa fedha wa 2015/16 halmashauri
yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinaathiri utekelezaji wa
malengo yaliyowekwa ikiwemo ucheleweshwaji wa fedha za ruzuku kutoka serikali
kuu pamoja na kutofikiwa kwa malengo ya
ukusanyaji mapato kwenye baadhi ya vyanzo vya halmashauri.
Kagoro alizitaja changamoto zingine
kuwa ni pamoja na kukosekana kwa fedha kutoka kwa wahisani kulikosababisha
miradi kama ya TACAIDS NA SEDEP kushindwa kutekelezeka pamoja na kuwepo kwa
matukio makubwa ya kitaifa yakiwemo maonesho ya kilimo ya nane nane na mbioza
mwenge ambazo hugharimu rasilimali fedha nyingi nje ya mpango wa Halmashauri.
Aidha mkurugenzi huyo aliomba
ushirikiano miongoni mwa watendaji pamoja na baraza la madiwani kwa ujumla ili
kuweza kufikia malengo yaliyowekwa katika mpango wa maendeleo na bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 huku akitoa wito
kwa watendaji wa idara ya fedha kufanya kazi kwa bidii katika ukusanyaji wa
mapato ya halmashauri.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Andrew Mtumusha aliwataka watendaji wa halmashauri ya mji
masasi kuwa na uwazi kwenye mapokezi ya fedha za miradi kutoka serikali kuu
pamoja na misaada ya wahisani sambamba na ushirikiano baina ya watendaji na
madiwani ili kufikia malengo mbalimbali yaliyowekwa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD