TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Mkuu wa
mkoa wa Mtwara Halima Dendego jana
amewaongoza mamia ya akinamama mkoani humo katika uzinduzi wa wiki ya wanawake duniani kwa kufanya usafi
katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula na kisha kuzindua zoezi la uchangiaji damu
salama.
Aidha
amewataka wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi kwenda kuchangia damu
kwenye viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara ili kuokoa maisha ya ndugu zao,jamaa
pamoja na marafiki hasa akinamama wajawazito na watoto.
Kwa mujibu wa mkuu huyo
wa mkoa alisema vitendo vya rushwa na urasimu wa tiba ya damu unaofanywa na
baadhi ya watumishi wa idara ya afya nchini ni sababu moja wapo inayoifanya
jamii kukata tamaa katika suala la kujitokeza kuchangia damu hivyo
kushindwa kufikia lengo la kukidhi mahitaji ya damu salama kwa asilimia 100.
Alisema wanawake na watoto ni kundi linaloathirika na tatizo la
ukosefu wa damu katika kwenye hospitali na vituo vya afya na kwamba ni vyema
serikali kwa kushirikiana na mpango wa Taifa wa damu salama ukaweka mazingira
yatakayosaidia kuokoa maisha ya kundi hilo muhimu kwenye jamii.
Dendego alisema kinachochangia kuwepo kwa upungufu wa damu ni matumizi ya damu yasiyo sahihi hospitalini
yanayofanywa na baadhi ya watumishi wa idara ya afya nchini wasio waaminifu.
“Ndugu zangu wana Mtwara
nawaomba mjitokeze kwenye zoezi la
kujitolea damu kwa hiyari katika maadhimisho haya ya siku ya wanawake duniani
ili tuokoe maisha ya akinamama na watoto ambao ndio waathirika wakubwa”.alisema
Dendego.
Alisema kuwepo kwa mpango wa Taifa wa damu salama kumesaidia kuondokana
kabisa na kutegemea wachangiaji wa kulipwa ama ndugu na jamaa wa wagonjwa ambao
wengi wao hawana vigezo vya kujitolea damu.
Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO) takribani wanawake 800 hufariki dunia kila
siku ulimwenguni kote wakati wa
kujifungua kutokana na matatizo ya damu ambapo takwimu zinaonesha kwamba wengi
wao ni kutoka kwenye nchi zinazoendelea na kwamba zaidi ya nusu ya vifo hivyo
huwapata akinamama waishio kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara.
Zoezi
hilo la uchangiaji wa damu,usafi pamoja
na shughuli mbalimbali za maendeleo zitafanyika
kwa muda wa wiki moja ambapo kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani
kitafanyika siku ya tarehe nane mwezi huu mkoani Mtwara ambapo kauli mbiu ya
mwaka huu ni uwezeshaji wanawake,tekeleza wakati ni sasa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD