TANGAZO
pichani ni mwili wa marehemu AVARIST ALFRED LUKANGA (28) A.K.A (MABLA) ukiwa kweye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mkomaindo. Kijana huyo ni mkazi wa kijiji cha Malolo Ruangwa Lindi ambaye ameuawa kwa kupigwa na watu wenye hasira kali na baadaye kuchomwa moto katika eneo la Rest Camp usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8:00 kwa kile kinachodaiwa kuwa ni tabia yake ya "WIZI" aliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu.Poleni sana kwa familia yake na pia kwa wakazi wooote wa kijiji cha Malolo.....
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Mkazi wa kijiji cha
Malolo,kata ya Malolo wilayani Ruangwa katika mkoa wa Lindi Evaristus Alfred
(27) ameuawa kwa kupigwa mapanga na mawe na baadae kuchomwa moto na wananchi
wenye hasira kali kwa tuhuma za wizi.
Tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 8:00 usiku katika eneo la Maendeleo mjini Masasi ambapo
marehemu alikamatwa wakati anajiandaa kuiba solar panel nyumbani kwa Bwana
Mboka kwa kupanda juu ya paa ya nyumba hiyo.
Jeshi la polisi mkoa
wa Mtwara kupitia kamanda wa mkoa huo Augustino Ollomi limethibitisha kutokea
kwa tukio hilo kwa kusema kwamba marehemu alikuwa ni miongoni mwa wahalifu
waliokuwa wanatafutwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi mkoani humo.
Alisema siku ya tukio
baada ya kukamatwa wananchi hao waliamua kumpiga kwa mapanga na hatimaye kumchoma
moto usiku huo ndipo baadhi ya wasamaria wema walipoamua kupiga simu polisi kwa
msaada zaidi.
Kamanda Ollomi
alisema mwili wa marehemu huyo ulifikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
hospitali ya Mkomaindo Mjini Masasi na baadaye ndugu wa marehemu waliitambua
maiti na walikabidhiwa kwa ajili ya mazishi.
Alisema tukio la kuuawa
kwa kijana limepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi wengi mkoani Mtwara
pamoja na Mkoa wa Lindi huku wengi wakionesha kuwa na furaha kutokana na kuuawa
kwa kijana huyo aliyekuwa na tabia ya wizi kwa kipindi kirefu.
Kwa upande wao wakazi
wa kijiji cha Malolo wilayani Ruangwa ambako ndiko mahali marehemu alikozaliwa wengi
waliohojiwa na gazeti hili walisema kuwa kwa sasa wataishi kwa amani na furaha
mara baada ya kifo cha kijana huyo ambaye kwao alikuwa ni kikwazo cha maendeleo
kijijini hapo.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD