TANGAZO
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA KUANZIA TAREHE 01-08/03, 2015 KUTAKUWA NA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
SHUGHULI MBALIMBALI
ZINATARAJIWA KUFANYWA KWENYE MAADHIMISHO HAYO IKIWA NI PAMOJA NA:
v UPIMAJI
WA SARATANI YA MATITI PAMOJA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE.
v UPIMAJI
WA VIRUSI VYA UKIMWI
AIDHA KATIKA
MAADHIMISHO HAYO YANAYOTARAJIWA KUAZIMISHWA KIMKOA KATIKA MANISPAA YA MTWARA
MIKINDANI PIA KUTAKUWA NA SHUGHULI ZA USAFI ZENYE LENGO LA KUUFANYA MJI WA
MASASI KUWA NI MIONGONI MWA MIJI INAYOZINGATIA KANUNI ZA USAFI WA MAZINGIRA
HIVYO WANAWAKE KWA KUSHIRIKIANA NA WANAUME,VIJANA WATASHIRIKI KWENYE ZOEZI LA
USAFI WA MAZINGIRA KAMA IFUATAVYO:
TAREHE 01/03/2015
USAFI UTAFANYIKA HOSPITALI YA MKOMAINDO MASASI
KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI.
TAREHE 2&3
MACHI,2015 WANANCHI WOTE
WANATAKIWA KUFANYA USAFI KWENYE MAENEO YAO WANAYOISHI HASA KWENYE KAYA ZENYE
MAHITAJI MAALUMU IKIWEMO WAZEE,WALEMAVU NA WAGONJWA.
TAREHE 04/03/2015 USAFI UTAFANYWA
KWENYE ENEO LA STENDI KUU MJINI MASASI KUANZIA
SAA 2:00 ASUBUHI.
TAREHE 05&06/03
WANANCHI WOTE MNAOMBWA KUJITOKEZA KUSHIRIKI USAFI KWENYE MAENEO YA KAYA ZENU.
TAREHE 07/03/2015 USAFI UTAFANYIKA
KWENYE MAENEO YA SOKO KUU LA MKUTI KUANZIA SAA 2:00 ASUBUHI.
KWA WAKAZI WA KATA YA SULULU UPIMAJI HUO WA SARATANI YA MATITI NA SHINGO YA KIZAZI UTAFANYIKA KWA KUFUATA RATIBA IFUATAYO:
§ 02/03/2015
UPIMAJI HUO UTAFANYIKA KIJIJI CHA MKAPUNDA “A”
§ 03/03/2015
WATAALAMU WA AFYA WATAKUWA KIJIJI CHA MKAPUNDA “B”
§ 04/03/2015
HUDUMA ZITATOLEWA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SULULU
§ 05/03/2015
MADAKTARI WATAKUWA MKARAKATE
§ 06/03/2015
NI KATIKA KIJIJI CHA MAKULANI
§ 07/03/2015
WAKAZI WA MTAKATENI WATAPATIWA HUDUMA
MKURUGENZI WA
HALMASHAURI ANAPENDA KUWAKUMBUSHA WAKAZI WA MJI WA MASASI KUWA KILA JUMAMOSI YA
MWISHO WA MWEZI NI SIKU YA USAFI AMBAPO KILA MWANANCHI ANATAKIWA KUFANYA USAFI
KATIKA ENEO LAKE ANALOISHI.
EWE MKAZI WA MJI WA
MASASI NA VITONGOJI UNAOMBWA KUJITOKEZA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WANAWAKE
KATIKA MAADHIMISHO HAYO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI AMBAYO KAULI MBIU YA MWAKA
HUU INASEMA:
“UWEZESHAJI
WANAWAKE, TEKELEZA WAKATI NI SASA”!!!!
WOTE MNAKARIBISHWAAAA!!!
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD