TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi
Mkazi wa mtaa wa
Wapiwapi Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara Kabura Joseph (35) ambaye
ni mfanyabiashara ya vinywaji amepigwa
risasi tatu mbili chini ya titi lake la kulia na nyingine moja mgongoni na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Tukio hilo la
kusikitisha limetokea jana majira ya saa 2:30 usiku katika eneo la Wapiwapi
karibu na geti la kuingilia nyumbani kwake wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa
akirejea kutoka kwenye biashara zake.
Kamanda wa polisi
mkoa wa Mtwara amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa majambazi
hayo yalimvamia mfanyabiashara huyo na kufanikiwa kupora mkoba wake ambao hadi
sasa haijafahamika kuwa kulikuwa na vitu gani ndani ya mkoba huo.
Kwa sasa majeruhi
yuko katika Hospitali ya misheni ya Ndanda Wilayani Masasi na kwamba tayari
mdaktari wamefanikiwa kutoa risasi mbili zilizokuwa chini ya titi lake la
kulia huku moja iliyo mgongoni ikisubiri hadi watakapomgeuza kwa ajili ya
upasuaji.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD