TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Mtwara.
Wakala
wa maabara ya Mkemia mkuu wa serikali GCLA imezindua jengo la maabara kwa kanda
ya kusini ili kusimamia na kuratibu shughuli zote zinazofanywa na taasisi hiyo
ili kusogeza huduma zake kwa wananchi.
Akizungumza
juzi mkoani Mtwara wakati wa uzinduzi wa jengo hilo mkemia mkuu wa serikali,
Profesa Samwel Manyele alisema jengo
hilo la maabara litakuwa likitumika katika uchunguzi wa vielelezo vya makosa ya
jinai.
Alisema
hitaji la kuongezwa kwa mkoa wa Mtwara ni kufanya uchunguzi wa
kimaabara kwa vielelezo vya makosa ya jinai zikiwemo za mauaji, ubakaji,
ujambazi kwa kutumia silaha na matumizi ya madawa ya kulevya sambamba na
uchunguzi wa sampuli zinazopelekwa maabara kwa kuhisiwa kuwa na sumu.
Kwa
mujibu wa Manyele alisema kituo hiko kitawapa fursa madaktari kuwahudumia vizuri na kwa mapema wale wagonjwa
wanaopelekwa baada ya kunywa au kuhisiwa kutumia matumizi ya vitu vyenye sumu.
Kwa
upande wake katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii, Dkt.Donnan Mmbando
alisema pamoja na jitihada ambazo
zimekuwa zikifanywa na serikali ili
kuleta ufanisi wa kiutendaji kwa maabara lakini bado kuna changamoto ikiwemo uchakavu
na ukosefu wa vifaa na mitambo ya kisasa.
Alieleza
kuwa ukosefu wa majengo, ufinyu wa
bajeti, pamoja na upungufu wa rasilimali watu ni changamoto zingine
zinazokwamisha utendaji bora wa maabara hizo nchini.
Aidha
alisema kuwa uwepo wa maabara hiyo kupitia utekelezaji wa shughuli za kisheria
na uchunguzi kutatoa matokeo yatakayosaidia mamlaka nyingine ya kisheria katika
kutoa maamuzi ambayo hupelekea utoaji wa haki hivyo kuleta utengamano katika
jamii.
Naye
Mkemia Mkuu wa Serikali meneja kanda ya kusini, Everlight Matinga, alisema kuwa
hitaji la kuanzishwa kwa maabara ya kanda ya kusini kunatokana na ukuaji wa
shughuli za uchumi na jamii ambazo zinahitaji utaalamu wa maabara ya mkemia
katika nyanja za usimamizi na udhibiti wa kemikali na uchunguzi wa ubora wa
bidhaa mbalimbali za viwandani na mashambani.
Mchakato
wa kuanzishwa kanda hii ulianza kwa kufanya upembuzi yakinifu kuhusiana na
mahitaji yakiyokuwepo ikizingatiwa kwa sasa mkoa wa Mtwara ni mkoa ambao
shughuli zake za kiuchumi na kijamii zinakuwa na zipo ambazo zinahitaji
utaalamu wa maabara ya mkemia mkuu ili kuondokana na ile changamoto ya kupeleka
sampuli mkoani Dar es Salaam.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD