TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Jeshi la polisi wilaya ya
Masasi mkoani Mtwara linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Maili sita kata ya Mtandi
Halmashauri ya Mji wa Masasi Daudi Pilipili (44) kwa tuhuma za kumlawiti mjukuu
wake wa kike (jina linahifadhiwa) mwenye
umri wa miaka tisa (13) anayesoma darasa la sita katika shule ya msingi Maili
Sita mjini humo.
Mkuu wa polisi wilaya ya
Masasi Azaria Makubi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio
hilo lilitokea jana majira ya saa 9:00 huko katika kijiji cha mailisita chooni
nyumbani kwa babu huyo aliyemlazimisha mjukuu wake kuhalalisha unyama huo
uliomsababishia maumivu makali.
Alisema mzee huyo alifanya
unyama nyumbani hapo akiwa peke yake kwa kuwa mke wake yaani bibi wa mtoto huyo
akiwa ameenda nyumbani kwa mwalimu mmoja
wa shule hiyo kwa ajili ya kuongea na kwamba alipoondoka alimwacha mumewe akiwa
na mjukuu wake.
Kwa mujibu wa Makubi
alisema kuwa mzee huyo amekuwa
akimwingilia kinyume na maumbile mjukuu wake na kwamba kila mara amekuwa
akimpatia fedha za matumizi ili kuficha tabia yake isiyokubalika kwe ye jamiii.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD