TANGAZO
Na Fatuma Maumba Mnyeto,Lindi.
Zaidi ya Vijana 200 wanaoshiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo wa
kujiajiri ambao wanatoka katika halmashauri sita za mkoa wa Lindi wamejiunga na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF ili waweze kupata huduma mbalimbali kutoka
ndani ya mfuko huo.
Akizungumza na gazeti
hili jana Meneja wa PSPF, mkoa wa Lindi, Ramadhani Mtumwa, alisema vijana wengi
wamevutiwa kujiunga na mfuko huo kutokana na mada ambayo aliyoitoa kwenye semina
hiyo.
Alisema katika kujikwamua
na umaskini wameweza kutoa mada kuwaelewesha namna gani vijana wataondokana na
umaskini hususani kupitia mfuko wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa
hiari ambao vijana wengi wamekuwa na mwamko mkubwa kutokana na faida
zinazopatikana katika mfuko huo.
Kwa mujibu wa Mtumwa
alisema Vijana wengi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kujiunga na mfuko kutokana
na faida zinazopatikana katika mfuko huo kama vile fao la elimu, fao
la ujasiriamani, fao la kujikimu katika maisha na mafao mengine hususani kwa
vijana ambao wanaokwenda kuanza maisha hasa hao ambao ni wajasiriamali.
Alisema kutokana na wengi
wa vijana hao kuwa na umri mdogo mfuko umeweka taratibu wa kuhakikisha kwamba wanaweza kujiwekea mafao pale watakapokuwa hawana uwezo wa kuweza
kuzalisha japo kuwa wapo kwenye fursa ambazo si rasmi kama wale ambao
wameajiriwa Serikalini ama katika mashirika ya umma.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD