TANGAZO
NaFatuma Maumba Wa Mnyeto,Lindi.
IMEELEZWA kwamba vijana ndio nguvu
kazi ya maendeleo ya uchumi wa taifa na kama hawatashirikishwa kikamilifu
katika shughuli za kijamii hasa kujiajiri wenyewe katika uzalishaji mali,
vijana wengi watajiingiza kwenye njia ambayo si sahihi .
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni mbunge wa jimbo
la Nachingwea, Mathias Chikawe wakati akifunga mafunzo ya siku 5 ya vijana ya
kuwajengea uwezo kuhusu kujiajiri iliyowashirikisha vijana 360 kutoka
halmashauri 6 za mkoa wa Lindi.
Chikawe amesema kwamba ni vizuri
Taifa likashirisha vijana katika utendaji kazi kwani usipomshirikisha kijana
kwenye shughuli za kijamii vijana wengi watajiingiza katika uvutaji wa bangi,
wizi pamoja na kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kuleva.
“Sote tunatambua kwamba walengwa wa
serikali hii ni vijana na tunatambua pia kwamba madhumuni ya semina hii
kuwawezesha vijana nyinyi kupata ufahamu na uelewa nafasi yenu katika jamii
wajibu wa vijana haki zao na kuwajengea uwezo na stadi za maisha.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa
Lindi, Mwantumu Mahiza, alisema kwamba mkoa umekusanya vijana hao wamalizapo
semina hiyo waelekee majumbani kwao na kila kijana aliyeudhurulia semina hiyo
akaunde kikundi chake kisichopungua vijana kumi kwa
malengo yanayofanana na kasha kujisajili.
Vikundi hivyo vitasimamia na watendaji
wa Kata, Maafisa Ugani, Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ushirika kwa
ajili ya kuviratibu na kuvipatia usajili kwa utamizi huo utakuwa chini ya
wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa kila halmashauri wa mkoa wa Lindi.
Mahiza alisema kuwa ili kuhakikisha kwamba vikundi hivyo
havitapagaranyika mara baada ya semina hiyo ameaandaa mkataba ambao atatiliana
saini makubaliano na wakuu wa wilaya“ Kila Mkuu wa wilaya kwa niaba yangu
katika ngazi na mamlaka niliyonayo kama atahakikisha vikundi hivyo vinaendelea
kama vikundi hivyo vitaparaganyika basi yeye ndio atakayewajibika.
Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao
wameshiriki mafunzo hayo Shamira Juma na Ali Bakari, wamemshukuru mkuu wa mkoa
wa Lindi, Mwantumu Mahiza kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia
kujikwamua kimaisha.
“Kwanza tunamshukuru mkuu wa Mkoa kwa
kutuwezesha vijana kwa kupata mafunzo mbalimbali sisi kama vijana tunachukua
fursa hii kwetu binafsi na vijana wenzetu uko tunakokenda tunaahidi viongozi
wetu na vijana wenzangu wasifikilie kama fursa hii kwetu imepotea sisi tutakua
chanzo au chachu ya maendeleo kwa vijana wenzangu katika kata zetu.
Mafunzo hayo ya siku tano
yaliyowashirikisha vijana 360 kutoka halmashauri 6 za mkoa wa Lindi, yalianza
rasmi February 23 hadi 27 mwaka huu lengo likiwa kuwajengea uwezo vijana hao wa
kuanzisha vikundi vya wajasiriamali vitakavyo wakwamua katika maisha yao ya
baadae.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD