TANGAZO
Manispaa ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika
chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya
maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za
wakazi wa eneo hilo.
Kazi hiyo
ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo, Kisiwani Kata ya
Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na wakishirikiana
na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya
Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi jioni, baada ya
kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye utafiti wakujua
tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani.
“Baada ya
kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo tulischukua jukumu la kwenda
kumhoji Mkuu wa washule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili
timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza kuwa alikuwa na akili
timamu,”alisema Tembo.
Alisema pamoja
na kuutekeza mlundikano huo wa kinyesi pamoja mikojo na matapishi bado
wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria
ili haki iweze kutendeka.
“Hili tukio
halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine ingawa hatuwezi
kuamini mambo ya ushirikina lakini haiwezekani mwalimu kama yule ajisaidie na
kuhifadhi uchafu kama ule ndani,”alisema.
Aidha, alisema
mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa
chumba chake uvunjwe chini ya uwaangalizi wa polisi.
Tembo, alisema
mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa
Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Haspitali ya Taifa muhimbili kwa ajili ya
kupimwa afaya baada ya kupata mshituko ambao umesababishwa na taarifa hizo.
Afisa Afya wa
Usafi wa Mazingira, Jumamne Muhogo, alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni
uchafu wa kinyesi, mikojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa
anatapika.
Pia alisema
kipo kifungu cha sheria, walifika pale maofisa kutoka idara mbalimbali kupima
uzito wa tukio, ambapo kama wangemkuta wangemkamata kwa hatua za kimfikisha
mahakamani.
Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza mahakamani.
Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza mahakamani.
“Tukio hili kwa
manispa ya Temeke ni la kwanza kutokea yani inaekekea huyu mtu hana akili ya
kawaida kama angekuwa na akili za kawaida asingeweza kufanya na mna
hii,”alisema.
Umati mkubwa wa
wakazi wa eneo hilo walikusanyika kwa wingi tangu saa tatu asubuhi wakisubiri
kazi hiyo hadi ilipofnyika saa tisa jioni na wataalamu wa manispaa hiyo.
Wataalamu hao
walimwagia dawa uchafu huo kisha kuanza ubeba na kutumbukiza chooni kwa
uangalifu mkubwa.
Walipomaliza
walivisafisha vyombo hivyo kwa kutumia dawa ambazo zimeweza kusaidia kuondoa
harufu mbaya iliyokuwa imezagaa hewani.
Awali, Sajenti
wa Jeshi la Polisi Ramadhan Kagolo, alisema aliwajibika kusimamia kuvujnjwa
kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kwa ajili
ya kulinda afya ya jamii.
Tukio hilo ambalo limekuwa likifuatiliwa na majirani hususan
jana wakati wa uteketezaji lilitokea Februari 22 mwaka huu.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD