TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego ameelezea kuridhishwa
kwake na jitihada zilizofanywa na Halmashauri ya mji wa Masasi katika
kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ililozitaka shule za sekondari nchini kuwa na maabara tatu za masomo ya sayansi.
Pia amepongeza umoja na mshikamano uliopo baina ya ofisi ya
mkuu wa wilaya ya Masasi na ofisi za wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji na ile
ya wilaya mazingira yanayopelekea wilaya hiyo kufanikiwa katika utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha ametoa agizo kwa wakuu wote wa shule za sekondari wilayani Masasi kuwapokea wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2014/2015
hata kama hawana sare pamoja na ada na kwamba ifikapo februari 15 mwaka huu
watoto wote wawe wameripoti shuleni.
Maagizo hayo pamoja na pongezi hizo alizitoa jana wakati wa
ziara yake ya siku moja ya kukagua ujenzi wa maabara kwenye shule kumi za
sekondari zilizopo Halmashauri ya mji wa Masasi ambapo amesema suala la ujenzi
wa maabara si ombi bali ni agizo halali la mkuu wa nchi na linapaswa
kutekelezwa na kila mtendaji wa Halmashauri husika.
Alisema wilaya ya Masasi ni miongoni mwa wilaya mkoani
Mtwara ambazo hadi sasa wanafunzi wengi waliochaguliwa kujiunga na kiidato cha
kwanza mwaka huu hawajaripoti shuleni licha ya serikali kujitahidi kuboresha
miundo mbinu ya shule hizo.
“Nawaagiza wakuu wa shule za sekondari mhakikishe kuwa
ifikapo februari 15 mwaka huu watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kwenye
shule zenu wawe tayari wamesharipoti…kinyume na hapo sitakuwa na msamaha na mtu
na nahaidi kufuatilia mimi mwenyewe mgugu kwa mguu suala hili kwa kuwa kwa
wilaya kama hii ni aibu kubwa”.Alisema Dendego.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya alisema kwa upande wa
ujenzi wa maabara ameridhishwa kwa kiwango kilichopo licha ya kuwepo kwa changamoto
kadhaa na ambapo ameagiza kwa shule ambazo maabara zake ziko kwenye hatua za
msingi zikamilishe kazi hiyo machi 30,mwaka huu huku kwa zile ambazo ziko
kwenye hatua ya upauaji zikamiike ifikapo februari 15,2015.
Dendego alisema Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo wa ndani na nje inapaswa kukamilisha ujezni wa maabara hizo pale
wakati utakapofika ili kuendana na agizo la Rais linaloishia Aprili mwaka huu.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD