Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

ANGALIA HAPA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE ZIARA YA MKUU WA MKOA WA MTWARA

TANGAZO


 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Othmani Dendego akitoa maelekezo kwa Ofisa mtendaji kata wa kata ya Sululu kuhakikisha kuwa watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2014/2015 wawe wameripoti ifikapo Februari 15 2015.


"Huyu ndiye Mkuu wa mkoa wa Mtwara anaitwa Halima Dendego maana watu wengine hamchelewi kuchanganya habari"(Ni maneno ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Masasi Kazumari Malilo-SIMBA WA YUDA akiwaambia wakazi wa Sululu.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiwa sambamba kabisa na mwenyeji wake mkuu wa wilaya ya Masasi Aijart Farida Mgomi alipowasili kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya kutwa ya Mwenge Mtapika wakati wa ziara yake ya kukagua maabara.

TANGAZA NASI KWA BEI NAFUU KARIBU NA BUREEEEE!!!!!!!

 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akipata maelezo ya awali kuhusu ujenzi wa maabara kutoka kwa mkuu wa shule ya sekondari ya kutwa ya Masasi mwalimu Jacksoni alipowasili shuleni hapo wakati wa ziara yake ya kikazi.
 Diwani wa kata ya Mtandi Albert Mlambala (mwenye suti) akimwongoza mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego katika kukagua maabara ya shule ya sekondari ya kutwa ya Mpindimbi Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara.
 Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiwaongoza kuimba wimbo maalumu wanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa  kata ya Mpindimbi
 TUIMBE WOTE KWA PAMOJA (RC MTWARA)

 Mkuu wa mkoa wa Mtwara akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mtandi (Hawako pichani ambapo ametoa ahadi kuwa kila mwananfunzi atakayemleta mwananfunzi mwenzake atampatia zawadi.
 Wanangu nawaomba msome kwa bidii kwani bila elimu ni tatizo katika maisha ni wosia alioutoa mkuu wa mkoa wa Mtwara wakati wa ziara yake kwenye shule ya sekondari ya kutwa ya Mtandi
 Pichani mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akiongea na wanafunzi wa sekondari ya mwenge mtapika.
 Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya mji wa Masasi akimwongoza mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego alipowasili kwenye shule ya sekondari ya Anna Abdallah iliyopo kata ya Napupa.
 Mkuu wa shule ya sekondari ya Mtandi mwl.Mpende akimwongoza mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego kufanya ukaguzi wa jengo la maabara linaloendelea kujengwa shuleni hapo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara pamoja na mwenyeji wake wakiwasili kwenye jengo la maabara shule ya sekondari ya Mtandi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro akimpa maelezo mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuhusu ujenzi wa maabara kwenye shule ya sekondari ya wasichana ya Masasi.
 

Hakikisha yote niliyokuagiza unatekeleza kikamilifu
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top