TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Lindi.
Wakuu wa wilaya wapya wametakiwa
kuacha tabia ya kukaa ofisini na badala yake waende kuwatembelea wananchi
katika maeneo yao ili waweze kujua matatizo yao.
Aidha wameombwa kutokata tamaa kutokana
na uchanga wao kwenye nyadhifa hizo
walizopewa na badala yake wapate muda wa kutosha wa kutembelea maeneo yao ya
kata na vijiji kwa lengo la kukutana na
wananchi ili wasikilize kero na malalamiko yao.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu
Mahiza alitoa kauli hiyo juzi wakati
akiwaapisha wakuu hao wapya wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea na kuwataka
kufanyakazi kwa ufanisi bila ya matatizo yoyote.
Alisema muda wa kukaa ofisini kwa
viongozi wa umma umekwisha ambapo amewataka kutembelea na kukagua miradi ya
serikali ambayo mabilioni ya fedha yameelekezwa huko kwa kuwa wananchi wana matarajio makubwa sana na
serikali yao.
Kwa upande wao wakuu wapya Mariam
Mtima Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa na Pololet Mgema, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
wamesema watahakikisha wanasimamia elimu, kilimo bora pamoja na afya
kuhakikisha vinaenda vizuri.
Walisema wanazo taarifa
kuwa suala la elimu liko chini sana na
kimsingi hata watoto ambao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu
ni asilimia ndogo tu ndio walioripoti na kwamba wamehaidi watahakikisha wanawahamasisha
wazazi wawaruhusu watoto wao wakapate elimu kwani hiyo ndio haki yao kwa ajili
ya maisha yao ya baadae.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD