TANGAZO
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ASHA MWETINDWA akisoma taarifa ya siku ya sheria nchini maadhimisho yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mahakama Hiyo. |
Na
Clarence Chilumba,Masasi.
Mahakama
ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara leo imeungana na mahakama pamoja na taasisi
zingine za kisheria nchini katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini katika
viwanja vya mahakama hiyo mjini humo huku mahakimu wakitakiwa kutenda haki sawa
kwa wananchi.
Akizungumza
kwenye maadhimisho hayo Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Masasi Asha
Mwetindwa alisema maadhimisho hayo yanafanyika kwa mara ya ishirini tangu
yalipoanzishwa mwaka 1996 ambapo kila mwaka huadhimishwa ifikapo mwanzoni mwa
Februari.
Maofisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Magereza wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini,aliyekaa kushoto kwa mkuu wa polisi Wilaya ya Masasi ni Ofisa Usalama wa Taifa wilaya ya Masasi Mwasiti Mfaume.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mahakama ya wilaya ya Masasi wakifuatilia kwa makini maadhimisho hayo.
Sheikh Suleiman Nasri kutoka Baraza la waislamu nchini (BAKWATA) akisoma dua kabla ya ufunguzi wa siku ya sheria nchini kwenye viwanja vya mahakama ya Wilaya ya Masasi.
Kaimu mkuu wa wilaya ya Masasi ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara akiongea na wafanyakazi,wageni waalikwa pamoja na wananchi wa kawaida wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
Tunawaweka Mikononi mwako wale wote wenye dhamana ya kutunga sheria,uwasimamie na kuwaongoza wote wanaogawa haki kisheria Vyombo vya mahakama,Majaji,mahakimu na watendaji wote Amina.(Rev:Fr.Dominick Mkapa wa kanisa katoliki parokia ya Masasi Jimbo la Tunduru Masasi.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
WAKILI WA KUJITEGEMEA AMBAYE PIA NI MWANASHERIA WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI SUBBY NZOA AKIWA NA MENEJA WA BENKI YA CRDB TAWI LA MASASI KWENYE VIWANJA VYA MAHAKAMA YA WILAYA YA MASASI WAKATI WA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD