TANGAZO
Na Hamisi Nasri,Masasi.
MKURUGENZI
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Beatrice Dominic
ameshindwa kutoa ufafanuzi mbele ya balaza la madiwani kuhusu makato ya sh.12
kwenye zao la korosho anayokatwa mkulima kwa kila kilo moja ya zao hilo kwa
ajili ya kuchangia ujenzi wa maabala baada ya kubanwa na madiwani wa
Halmashauri hiyo waliotaka kufahamu utaratibu uliyotumika kuhusu makato hayo.
Hata
hivyo mkurugenzi huyo baada ya kupatwa na kigugumizi kuhusu hoja hiyo
alilazimika kueleza wazi mbele ya balaza hilo kuwa kuhusu makato hayo anayefahamu
kwa kina ni mkuu wa wilaya hiyo Farida mgomi jambo ambalo madiwani hao waligeuka
kuwa mbogo na kuanza kumshambulia kwa maswali ili kupata ufafanuzi mzuri zaidi.
Mjadala
huo mkali baina ya madiwani hao na mkurugezi huyo ulifanyika jana katika kikao
cha balaza la madiwani wa Halmashauri hiyo na kwamba hoja hiyo ilikuja wakati
wa maswali ya papo kwa papo kikao hicho kilifanyika wilayani hapa.
Wakizungumza
kwa uchungu kwa niaba ya madiwani wenzao,diwani wa kata ya Mpindimbi ,Samsoni
Bushiri na Eduward Mahelela wa kata ya Chikoropola walisema kuwa hatua ya
Halmashauri kuvitumia vyama vya msingi kumkata mkulima wa korosho sh.12 iii
kufanikisha ujenzi wa maabala bila ridhaa yao ni jambo la kumnyonya kiuchumi
mkulima.
Aidha
madiwani hao walihoji utaratibu uliyotumika wa kuvipa dhamana vyama msingi na
wadau wa maendeleo kupanga makato ya sh.12 kwa mkulima kwa ajili ya kuchangia
ujenzi wa maabala.
“Utaratibu
uliotumika kumkata mkulima sh.12 kuchangia ujenzi wa maabala umekiuka utaratibu
wa balaza la madiwani kwa sababu sisi kama madiwani hatujashirikishwa kwenye
mchakato huu tunaomba utaratibu huu usitishwe,”walisema madiwani hao
Kwa
upande wake mkurugenzi huyo Dominic alisema katika mpango wa ujenzi wa maabala
kupitia fedha za mapato ya ndani Halmashauri ilitakiwa kuchangia kiasi cha
fedha sh. milioni 800 kwa msimu wa fedha unaomalizika Halmashauri ingechagia
sh. milioni 400 na kwamba kwa mwaka wa fedha ujao pia ingepata sh. milioni 400
ili kukamilisha ujenzi wa malaba hizo.
Alisema
kuwa pia Halmashauri ilipangilia kupata fedha kutoka kwenye vyama vya msingi (AMCOS)
ambapo vyama hivyo vilitakiwa kutoa fedha zaidi ya milioni 300 kwa maana ya
kwamba vyama hivyo kwa mwaka huu wa fedha vingetoa milioni 150 na kwa mwaka
ujao wa fedha pia vingetoa milioni 150 kuchangia ujenzi wa maabala.
Dominic
alieleza kuwa Halmashauri hiyo pia iliainisha kupata fedha kutoka kwa wadau mbalimbali
wa maendeleo wakiwemo taasisi, Mashirika,makampuni binafsi na watu binafsi
kuchangia zaidi ya milioni sh.800
“Mimi
kama mkurugenzi siwezei kuwa na majibu kuhusu hizi sh.12 zinatoka chanzo gani
mheshimiwa mwenyekiti siwezi kuwa na majibu kwa sababu mimi napokea hundi tu
ambayo haionyeshi shilingi ngapi kwa kilo na haionyeshi zimelipa shilingi ngapi
huo mchngo,”alisema Dominic
Alisema
suala la makato ya sh.12 kwa kila kilo ya mkulima kuchangia ujezi wa maabala lipo
mikononi mwa mkuu wa wilaya Farida Mgomi ndiye anayepaswa kuhojiwa na kutoa
ufafnuzi juu ya makato haya ni mkuu wa wilaya hivyo alishauri madiwani hao
kuunda kamati ndogo kwenda kwa mkuu wa wilaya ili kuhoji kwa kina zaidi suala
hilo.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD