TANGAZO
SHUKRANI KWA
WANANCHI WA MASASI
NDUGU zangu
wananchi wa Masasi ninachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa
kipindi chote cha takribani miaka mitatu nikiwa mkuu wa wilaya yenu. Nina kila
sababu ya kuwashukuru kwa kuwa ninyi mmenifanya niwe mkuu wa wilaya kweli. Upendo
na ushirikiano mkubwa kutoka kwenu ndio uliopelekea
mafanikio makubwa katika wilaya ya masasi na sasa utaiona Masasi inavyopaa.
Kwa kipindi chote cha uongozi wangu nikishirikiana nanyi nimefanikiwa kuondoa
njaa Masasi, kupunguza mimba za utotoni shuleni msingi na sekondari, kuongeza
uzalishaji wa korosho na mazao mchanganyiko, kuimarisha vyama vya ushirika wa
mazao, kuongeza ufaulu pamoja na kushinda nane nane kitaifa mwaka 2014.
Aidha katika
kipindi cha uongozi wangu tulifanikiwa kushinda mapokezi ya mbio za mwenge kikanda
kutoka nafasi ya mwisho 2012 hadi ya kwanza 2013, kupandisha timu ya Ndanda FC
kucheza ligi kuu ya vodacom, ujenzi wa barabara mjini hadi kufikia kiwango cha
lami barabara ya mkapa.
Ndugu zangu wana
masasi mafanikio mengine katika kipindi changu ni pamoja na ujenzi wa daraja la Nangoo ambalo lilisombwa
na maji wakati wa mafuriko mwaka 1990 ambalo limejengwa ndani ya mwaka na
kukamilika 2014, uimarishaji wa huduma za maji kupitia Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA) ambapo imepunguza tatizo la
maji kwa asilimia 80 kutoka ndoo moja ya lita 20 kuuzwa kwa shilingi 1000 kwa
mashaka hadi shilingi 50.
Uboreshaji wa huduma za umeme kwa kubadilisha nguzo
za zamani na kuweka mpya ili kupunguza kukatikatika kwa umeme hasa mwezi
desemba sambamba na hilo uwekaji wa umeme vijijini, uboreshaji wa zahanati na
vituo vya afya hasa chiwale baada ya kuongeza huduma za upasuaji hapo kijijini
chiwale, kuimarisha umoja wa waendesha bodaboda na kuwaanzishia saccos,
kuimarisha vikundi vya kina mama vya ujasiriamali, kuwapa vijana mashine za
kufyatulia tofali pamoja na mafunzo ili wawezekujipatiakipato,
Kushiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo
ujenzi wa maabara ambao umeshakamilika kwa zaidi ya asilimia 80, KUBWA KABISA
NA LA KUJIVUNIA NI UANZISHAJI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI AMBAYO
NILIIZINDUA TAR 2 DEC 2012 AMBAYO IMEBORESHA WILAYA YA MASASI NA KUIFANYA KUWA
MJI WA KIPEKEE KUSINI MWA TANZANIA UNAOKUWA KWA KASI KILA SIKU, kuanzisha
vyombo vya habari ikiwemo Radio FADHILA, kuanzisha chuo cha maendeleo kwa level
ya certificate na diploma QUALITY DEVELOPMENT COLLEGE, kushirikiana na
wafanyabiashara kuboresha mazingira
ya kibiashara kwa vikao nk.
Hayo ni sehemu
ya makubwa ambayo nilipokuwa kiongozi wenu hapo masasi niliweza ya kuyafanya
kwa ushirikiano na wananchi wa masasi.
Mwisho niwashukuru wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama,
mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mama Beatrice Dominick, mkurugenzi
wa Halmashauri ya mji Bwana Fortunatus Kagoro, mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya Bw. Juma Satma, mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Bw. Andrew Mtumusha,
wakuu wa idara Halmashauri zote, WAHESHIMIWA MADIWANI WOTE, watumishi wote,
viongozi wa taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali, viongozi wa AMCOSS
na MAMCU viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya kisiasa, wazee maarufu
na bila kuwasahau watu mashuhuri akiwemo Peneza _
Macapo , Wanyumbani,Aziz _Mkutti filling station , Yusuph- Muzdalfah n.k.
Nimeondoka Masasi nikiwa nimejenga team bora ya
ushindi kati ya serikali na wananchi wake kupitia vyombo vyake ikiwemo Halmashauri.
Nitaikumbuka Masasi daima kwani imenijenga na kunipa uzoefu nitawamiss sana
Masasi ni nyumbani tuendelee kuwasiliana.
Ninawapenda sana endeleeni kuniombea ili niweze
kutimiza majukumu ya serikali kupitia wilaya ya Chamwino. Kauli mbiu ya
aliyekuwa mkuu wa wilaya yenu Farida Mgomi isemayo “TUMEKUJA KIVINGINE KIKAZI ZAIDI” nawasihi msiiache. Ninawapenda
saanaaa MASASI OYEEEEEEEEE!!!!!!
MWISHO……
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD