TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Mbunge wa Jimbo la Mtwara
Vijijini, Hawa Ghasia amewataka wananchi na wanachama wa chama cha Mapinduzi wa Kijiji
cha Mbemba,Kata ya Mbemba, wilaya ya Mtwara Vijijini, kukichagua kwa kishindo chama cha
Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Rais na Wabunge sambamba
na kuipigia kura ya ndio Katiba
inayopendekezwa.
Hayo aliyasema juzi wakati anaongea na wananchi wa Kata ya
Mbemba kulikofanyika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa chama cha Mapinduzi(CCM)
pamoja na kusherekea ushindi wa kishindo walioupata Kata hiyo katika uchaguzi
wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.
Ghasia alisema mwaka 2015 wanatakiwa wajipange Kata yote ya Mbemba irudi tena
ndani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Jimbo la Mtwara Vijijini nalo lirudi
ndani ya chama hicho.
Alisema katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2009 Kata ya
Mbemba ilipata viti vitatu huku vyama vya upinzani wakifanikiwa kuchukua vijiji viwili na CCM kupata kijiji kimoja.
Kwa mujibu wa Ghasia alisema katika uchaguzi wa mwaka jana katika vijiji vitano
vya kata hiyo CCM walifanikiwa
kujinyakulia vijiji 4 huku vyama
upinzani vikiambulia kijiji kimoja tu na
kwamba kwa hali ilivyo kwa sasa wana imani kuwa kabla ya kufikia 2019 hata hiko kiti kimoja walichonacho
watakichukua.
“Ndugu zangu mwaka 2015
tujipange Kata yetu ya Mbemba irudi tena ndani ya chama cha mapinduzi na jimbo
letu la Mtwara vijijini nalo lirudi ndani ya chama tawala, hatuijui Katiba
itasemaje lakini kama Katiba hii haitaweza kutumika katika uchaguzi unaokuja
tukirudi kwenye Katiba ile ile jimbo hili litagawanyika mara mbili Nanyamba na
Mtwara Vijijini…Kwa hiyo tunaomba majimbo yote mawili yaende kwenye chama cha
mapinduzi na bado likibaki jimbo moja nalo lirudi kwenye chama chetu pia”.Alisema
Ghasia huku akishangiliwa.
Katika hatua nyingine Ghasia aliwataka wananchi hao kuhakikisha
katika uchaguzi wa mwezi Oktoba mwaka huu wanamrudisha mbunge wao makini pamoja
na madiwani na Rais kwa ujumla kutoka chama makini na chenye kujali wananchi
wake wengine waache wasage lami CCM mbele kwa mbele.
“Nawaomba mjitokeze kwenye
zoezi la kujiandikisha litakapoanza
kwenye maeneo yenu nendeni mkajiandikishe ili muweze kuipigia kura Katiba
inayopendekezwa pamoja na kuwapigia kura Rais, Wabunge na Madiwani katika
uchaguzi mkuu wa Mwaka huu 2015…
Mwaka huu tunatumia mfumo tofauti na miaka mingine kwa hiyo
usijidanganye kama nina kadi ya zamani haitatumika tena kwa hiyo
usipojiandikisha mwezi huu ujue hiyo imetoka hutoweza kuipigia kura Katiba mpya
inayopendekezwa na wala utowapigia kura Wabunge, Rais na Wabunge”.
Kwa upande wake, Jafari
Hassani, mbaye ni Mwanachama wa chama hicho, aliwashukuru wananchi wa Kata ya
Mbemba kwa kuichangua CCM kwa kishindo na waendelee hivyo hivyo mpaka kwenye
uchaguzi Mkuu ujao.
“Wananchi mlichokifanya mwaka
jana kwenye uchaguzi wa Serikali ya Mitaa endeleeni hivyo hivyo kwenye uchaguzi
Mkuu kwani hii ndio safari ya kuelekea kwenye maendeleo…Kamwe kusitokee kidudu
mtu akaja kutudanganya kwa hili, Ukawa wenyewe wameanza kupasuka kwani Ukawa ni
sehemu ya watu kutafuta kupiga pesa tu si kwa ajili ya kuleta maendeleo na
amani ya kweli ya wewe mwananchi wa hapa, alisema Jafari na kuongeza:
“Ndugu zanguni vyama vya upinzani ni sumu nadiriki kutamka hivyo
kwani vyama vya upinzani tulivyonavyo Tanzania ni sumu na sumu hata siku moja
haiuzwi, kama tunahitaji elimu, maji, hospitali na kilimo tulime tuvune tuuze
tupate pesa basi tuendelee kukiamini chama cha mapinduzi”.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD