Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

TAMKO LA SERIKALI YA WILAYA YA MASASI KUHUSU WAFANYABIASHARA KUFUNGA MADUKA KESHO

TANGAZO
Ndugu Wananchi leo tarehe 10/02/2015 kamati ya ulinzi na usalama imefanya kikao cha dharura na viongozi wa wafanyabiashara baada ya kusikia kuwa wafanyabiashara hao watasitisha kutoa huduma kwa kufunga maduka kesho tarehe 11/02/2015 wakishinikiza serikali juu ya tatizo la kiongozi wao wa kitaifa Bwana MINJA  ambaye kesho atakuwa anafikishwa mahakamani imjini Dodoma.
Baada ya majadiliano ya pande zote mbili maamuzi yafuatayo yamefikiwa ikiwa ni pamoja na:

  • HUDUMA ZA MADUKA ZIENDELEE KAMA KAWAIDA.
  • KAMA KUTATOKEA WATU  AMBAO WATAAMUA KUSITISHA HUDUMA WASIWALAZIMISHE WAFANYABIASHARA WENGINE AMBAO WATATAKA KUFUNGUA MADUKA NA KWAMBA KWA KUFANYA HIVYO NI KINYUME NA SHERIA NA HATUA KALI ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.
  • YULE ATAKAYEFUNGA AFANYE HIVYO BILA KUMSHAWISHI MWINGINE AU KUFANYA KITENDO CHOCHOTE CHA UCHOCHEZI WA MANENO AU VITENDO.
  • RAI ya serikali wilaya ya Masasi ni kuwataka wafanyabiashara kuendelea kutoa huduma na kwamba kesi ya Bwana Minja inashughulikiwa kwa mujibu wa sheria na si kuwanyima huduma wananchi wa Masasi. 
  • TUDUMISHE MSHIKAMANO,UMOJA NA AMANI KATIKA WILAYA YA MASASI,NI WITO WANGU KUWA TUTAENDELEA KUDUMISHA AMANI KWA MAENDELEO YETU.
NI MIMI FARIDA .S. MGOMI
MKUU WA WILAYA YA MASASI
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top