Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU VYA MASOMO YA SAYANSI MTANDI SEKONDARI-HALMASHAURI YA MJI MASASI.

TANGAZO
 Na Clarence Chilumba,Masasi.

Kampuni ya mawasiliano hapa nchini ya Airtel imetoa  msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya kutwa ya Mtandi Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara vyenye thamani ya shilingi milioni moja  kwa lengo la kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha tatizo la masomo ya sayansi linabaki kuwa historia.

Airtel pia kupitia mpango wake wa shule yetu imedhamiria kuwapatia wanafunzi wa shule za sekondari Halmashauri ya Mji wa Masasi mazingira bora ya kujifunzia kwa kutoa vifaa vya kufundishia mashuleni ikiwemo vitabu vya ziada na kiada na kwamba hadi sasa tayari shule zaidi ya 900 nchini zimenufaika na mpango huo.

Aidha kampuni hiyo inayolenga kuleta maisha ya kidijitali katika jamii ya Watanzania imeandaa mpango mkakati utakaosaidia kuongeza kiwango cha ufaulu katika masomo ya sayansi kama vile Baiolojia,Kemia pamoja na Fizikia kwa kutoa vitabu vya sayansi kwa shule zenye uhaba wa vitabu hivyo.

Akizungumza hii leo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada huo meneja wa Airtel mkoa wa Mtwara Barthlomew Masatu alisema kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na  serikali imeandaa mikakati mbalimbali itakayosaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini hususani tatizo la masomo ya sayansi.

Alisema suala la kukosekana kwa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule nyingi za sekondari nchini  kumechangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu wa masomo hayo hali ambayo ikiachwa iendelee nchi ya Tanzania  itakosa wataalamu  wa sayansi wakiwemo madaktari,mainjinia pamoja na wataalamu wa gesi asilia.

“Mpango huu wa “shule yetu” ni endelevu… na kwamba kwa mwaka huu tutashuhudia shule nyingi za sekondari zikifikiwa na mpango huo hivyo ni matumaini yangu kuwa msaada huu utaleta tija na mabadiliko katika jamii yetu kwani elimu ndio msingi wa maisha”.alisema Masatu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha aliishukuru kampuni ya Airtel kwa kuonesha njia kwa makampuni mengine makubwa hapa nchini ili yaweze kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhakikisha kila mwanafunzi mmoja anatumia kitabu kimoja.
Mwisho.

Meneja wa Airtel wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mr.Kijuu akimkabidhi kitabu mkuu wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mtandi Mwl.Humud Mpende. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi FORTUNATUS KAGORO kulia akipokea msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka kwa  meneja wa kampuni ya Airtel wilaya ya Masasi.
 Meneja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Bwana BARTHLOMEW MASATU akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya kutwa Mtandi Halmashauri ya mji wa Masasi
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi ANDREW MTUMUSHA akimkabidhi kitabu kaka mkuu wa sekondari ya kutwa ya Mtandi kitabu ikiwa ni ishara ya kupokea msaada huo kutoka kwa kampuni ya Airtel.
 Wanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mtandi wakitoa burudani wakati wa Hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi kwa shule ya sekondari ya kutwa ya Mtandi.


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi FORTUNATUS KAGORO akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu kutoka kwa kampuni ya Airtel.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi ANDREW MTUMUSHA akiongea kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitabu kutoka AIRTEL.







TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top