TANGAZO
WENYEVITI WA VIJIJI,VITONGOJI WAONYWA KUJIGEUZA MIUNGU WATU.
Na
Clarence Chilumba, Masasi.
Wenyeviti
wa serikali za vijiji na vitongoji katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi
mkoani Mtwara wametakiwa kufuata kanuni na sheria za nchi katika kutekeleza
maamuzi yao katika maeneo yao ya kazi huku wakiaswa kuacha tabia ya kujifanya
miungu watu.
Aidha
wameagizwa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ya utawala ili
kuiwezesha Halmashauri hiyo kukusanya mapato yatakayotumika kuwahudumia
wananchi katika huduma mbalimbali za kijamii.
Pia
wamekumbushwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya utawala bora huku wakionywa
kuacha kufanya maamuzi yao binafsi na badala yake wafanye maamuzi yao katika
misingi ya ushirikishaji, uwajibikaji na kwamba kwa kufanya hivyo watapunguza
malalamiko ya wananchi.
Akizungumza leo mbele ya wenyeviti hao wa vijiji na vitongoji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi
mkuu wa wilaya ya Masasi Farida Mgomi
alisema wanapaswa kutambua kuwa majukumu waliyopewa na wananchi ni makubwa na
kwamba ni muda muafaka kwa wao kuanza kuwahudumia wananchi hao.
Alisema
serikali za vijiji na vitongoji ni serikali kamili na zenye mamlaka kamili
lakini changamoto kubwa iliyopo kwa baadhi ya watendaji hao ni pale
wanapojigeuza kuwa miungu watu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa hatosita kumchukulia mtendaji yoyote wa ngazi ya
kijiji au kitongoji kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na ndio maana
serikali imeweka utaratibu mpya kwa wenyeviti hao kula kiapo mbele ya
mwanasheria.
Alisema
huu si wakati wa kuleta porojo katika utekelezaji wa majukumu ya msingi kwa
jamii na kwamba ni lazima wawatumikie wananchi kikamilifu kwani wakati wanaomba
ridhaa ya kuongoza walitoa ahadi kemekemu hivyo ni lazima wazitimize ahadi
walizozitoa ili kurudisha imani kwa waliowachagua.
Naye
mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Beatrice Dominick alisema wameandaa
kikao hicho cha kazi ili kutoa maelekezo
pamoja na muongozo kwa wenyeviti hao wa vijiji na vitongoji ili waweze
kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwenye maeneo yao.
Mwisho.
Kutoka kushoto: Katibu tawala wa wilaya ya Masasi Dunford Peter,Mkuu wa wilaya ya Masasi Farida Mgomi,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Juma Satma pamoja na makamu wa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Chilala wakifuatilia zoezi la kuapishwa kwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji wa Halmashauri ya wilaya ya Masai Hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Emirates mjini Masasi.
Baadhi ya wenyeviti hao wa vitongoji na vijiji wakifuatikia maelekezo kutoka kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Beatrice Dominick
Viongozi mbalimbali wa wilaya ya Masasi wakiaagana na mkuu wa wilaya ya Masasi nje ya ukumbi wa mikutano wa Emirates mjini Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD