TANGAZO
BAKWATA:VIONGOZI WA SIASA ACHENI KUPOTOSHA JAMII
Na Clarence Chilumba,Masasi
Baraza la
waislamu Tanzania (Bakwata) wilayani Masasi limewaonya viongozi wa vyama vya
siasa hapa nchini kuacha mara moja njama zao chafu pamoja na tabia ya
kuwapotosha wananchi hata kwenye masuala ya msingi kwa Taifa na badala yake ni
vyema wakatumia muda mwingi kueleza sera zao kwa wananchi.
Aidha baraza hilo
limeelezea kusikitishwa na kushangazwa kwake na kauli zinazotolewa na baadhi ya
viongozi wa vyama vya siasa hapa nchini kwamba endapo vyama vyao vitashindwa
kwenye uchaguzi mkuu ujao basi ni dhahiri kuwa nchi haitatawalika kwa sababu tu ya vyama vyao
kukosa ushindi.
Pia vyama hivyo
vimeaswa kuachana na dhana kuwa kwa kushawishi vijana kufanya fujo pamoja na
maandamano ni sera ambazo zinazoweza kuwapeleka ikulu na kwamba ni vyema
watambue kuwa kwenye uchaguzi wowote hapa duniani mshindi hupatikana kwenye
sanduku la kura.
Kauli hiyo
imetolewa jana wilayani hapa na katibu wa Bakwata wilaya ya Masasi Ustaadh
Hamisi Baina alipokuwa anazungumza na gazeti hili ofisini kwake juu ya maoni na
mtazamo wa baraza hilo kuelekea kwenye zoezi la katiba inayopendekezwa pamoja
na uchaguzi mkuu mwezi oktoba.
Alisema baadhi ya
viongozi wa vyama vya siasa hudhani kuwa kwa kufanya vurugu huku wakitu ia mabavu ni njia muafaka ya kuongoza nchi na kwamba hiyo si kweli na kwamba kwa kufanya
hivyo kutaelekea kuvunjika kwa amani ambayo ni lulu kwa Taifa letu la Tanzania.
Kwa mujibu wa
Baina alisema kuwa viongozi wa vyama hivyo wana wajibu wa kuzungumza sera zao
kwa wananchi ambapo pia waache tabia ya kukashifu na kukosoa jitihada kubwa
zinazofanywa na serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Alisema
kuibuka kwa matukio ya uvunjifu wa amani hapa nchini ni baadhi ya matokeo ya baadhi
ya viongzoi wa vyama vya siasa kutokuwa na hofu dhidi ya mungu ambapo wengi wao
wakiwa wamekosa kuwa na maadili ya kimungu.
Akizungumzia
kuhusu madai ya watu kudai kuwa viongzoi wa dini wamekuwa wakitumia muda mwingi
kuzungumzia masuala ya serikali badala ya waumini wao, Baina alisema kiongozi
yeyote wa dini mwenye utashi ni lazima aishauri serikali kwa yale mambo yanayoweza
kuiingiza nchi kwenye machafuko.
“Vitabu
vya dini vinasema kuwa itii mamlaka iliyopo madarakani lakini wanapokosea ni
lazima viongzoi wa dini lazima tuishauri serikali…na si kwamba tunaiongzoa au
tunaingilaia kazi zao”. Alisema.
Kuhusu
katiba inayopendekezwa alisema kuwa wananchi wenyewe waachwe waamue kuikaubali
ama kuikataa katiba hiyo na kwamba maamuzi yao binafsi baadhi ya viongozi wa
vyama vya siasa yasililiingize Taifa kwenye mambo yale yatakayolipeleka kwenye
machafuko
Alisema
anashangazwa na viongozi wanaowadanganya watu kuwa rasimu ya jaji warioba
ilitakiwa isijadiliwe kwenye bunge maalumu la katiba bali ilitakiwa ipitishwe
ambapo amesema jambao hilo lisingewezekana kwani rasimu ni lazima ijadiliwe ili
kufikia maamuzi.
Baina
alisisitiza kuwa jamii ya watanzania inapaswa kuacha mara moja vitendo vya
kikatili ambavyo vimekuwa vingi hapa nchini wanavyofanyiwa watoto, akinamama na
wazee na kwamba wanapaswa kumrudia mungu.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD