Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

TANGAZO

Mwenyekiti wa PAC Zito Kabwe akihutubia wananchi
UKAWA WAWASHA MOTO MTWARA
Na Clarence Chilumba,Mtwara.
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashirika ya umma zito kabwe amewataka wananchi kuondoa wasiwasi dhidi ya watuhumiwa wa kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow ambao hawajachukuliwa hatua kuwa bunge lijalo litahakikisha maazimio yote nane yaliyopelekwa kwa Raisi yanatekelezwa bila ya ukinzani wowote.

Akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mikoa ya kusini katika uwanja wa mashujaa mjini mtwara zito kabwe ambaye aliombwa na chama cha wananchi CUF kutoa ufafanuzi juu ya kashfa hiyo alisema haoni sababu ya maazimio ya bunge dhidi ya watuhumiwa hao kutotekelezwa kikamilifu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CUF Taifa profesa Ibrahimu lipumba amewashukuru wananchi wa mikoa ya kusinii kwa kukichagua chama cha CUF katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika Desemba142014.
 Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Lindi mjini kupitia chama cha wananchi CUF Mohamedi  Baruani  alisema kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa wananchi wa mikoa ya kusini wameonesha kutuunga mkono na kwamba wana imani kuwa katika uchaguzi  mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu watashinda kwa kishindo.

Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi wa wilaya zote za mikoa ya lindi na Mtwara  ulianza kwa maandamano yaliyozunguka  mitaa  kadhaa ya Manispaa ya mji wa  mtwara.
Mwisho.


 Maelfu ya Wananchi wa manispaa ya Mji wa Mtwara wakimisikiliza mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mashirika ya umma (PAC) Zito Zuberi Kabwe kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mtwara
.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba akiwasha moto kwenye viwanja vya mashujaa.

Wananchi wakifuatilia mkutano huo

 Mbunge wa CUF akiongea na wana Mtwara


Viongozi waandamizi wa UKAWA wakiwa jukwaani wakifurahia burudani kutoka kwa msanii maarufu kanda ya kusini "KUNDAMBANDA"(hayuko Pichani).

VIJANA nao hawakuwa nyuma katika kufuatilia hotuba za viongozi wa UKAWA mjini Mtwara

 Msanii maarufu mkoani Mtwara anayeimba nyimbo zake kwa Lafudhi ya kabila la kimakonde KUNDAMBANDA akitoa burudani kwa wanachama na mashabiki wa UKAWA kwenye viwanja vya mashujaa mjini Mtwara
 Kiongozi wa UKAWA akihutubia wananchi wa Mtwara

Kigogo wa UKAWA akifanya vitu vyake kwenye mkutano wa Hadhara mjini Mtwara

Vijana wakifuatilia mkutano huo kwa umakini wa hali ya juu


Kabwe ZitoZuberi
 Akinamama nao hawakuwa nyuma kufuatilia mkutano huo wa UKAWA

Mmoja wa kiongozi mwanamke wa UKAWA akitoa somo kwa wanawake wenzake

Mashabiki na wanachama wa UKAWA

 Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba

Peoples' Power
Burudani nazo hazikuwa nyuma 

 Mashabiki wa UKAWA wakifuatilia mkutano huo
KUNDAMBANDA akifanya yake mkutanoni

Viongozi wa UKAWA

" &HAKI SAWA KWA WOTE"& PEOPLE'S POWER'

Miongoni mwa viongozi wa UKAWA wakimwaga cheche zao mkoani Mtwara

Zito Zuberi Kabwe ndani ya viwanja vya mashujaa mjni Mtwara

 Mbunge wa Jimbo la Lindi kupitia chama cha wananchi CUF Mohamedi Baruani naye akitoa somo kwa wana Mtwara ambapo pia alitumia muda huo kuwashukuru wana mtwara kwa kuichagua CUF kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa.


Wanachama wa UKAWA

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top