TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Mtwara.
Kitendo cha baadhi ya
wavuvi kujihusisha na uvuvi haramu wa kuvua kwa kutumia baruti ni jambo
linalotakiwa kukabiliwa kwa nguvu zote ili kuhakikisha tatizo hilo linamalizika
sambamba na kuendelea na kuhifadhi mazingira ya bahari na viumbe vilivyomo.
Aidha imebainika kuwa
watu wengi wanaoishi katika hifadhi ya bahari wamekuwa wakiendesha maisha yao
ya kila siku kwa kutegemea rasilimali za bahari lakini wengi wao wamekuwa
wakijihusisha na uvuvi haramu wa kutumia mabomu na nyavu ndogo kinyume na
sheria.
Hayo yalisemwa na Naibu waziri wa Wizara ya Maendeleo
ya Mifugo na Uvuvi Kaika Telele wakati wa ziara yake ya kikazi katika mikoa ya
Lindi na Mtwara kufuatia kupewa taarifa
na wahifadhi wa bahari juu ya vitendo
vya kiuhalifu vinavyofanywa na wavuvi katika mikoa hiyo.
Alisema vitendo vya uvuaji haramu ni jambo ambalo
halipaswi kufumbiwa macho kwani linahatarisha maisha ya viumbe walio baharini
pamoja na kuharibu uhifadhi wa mazingira hivyo ni vyema sasa mswada ukapelekwa
bungeni ili wahusika washtakiwe kama wahujumu uchumi.
“Hili jambo la uvuvi kwa
kutumia baruti ni baya kuliko kwa nini mswada usipelekwe bungeni hao watu
wakawa kama wahujumu uchumi moja kwa moja ambayo hawawezi kupata dhamana maana
hata kwenye mahakama zetu bado kuna tatizo kesi zinakaa miaka kadhaa hivyo kuwakatisha
tama wale watendaji”.Alisema Telela.
Akisoma taarifa ya
hifadhi ya bahari ya huba ya mnazi na maendeleo ya mto Ruvuma
(Marine Park) mhifadhi Alfred Ngowo alisema katika kipindi cha mwaka 2013/2014
pamoja na nusu mwaka 2014/2015 zilifanyika doria 41 ili kuzuia uvuvi haramu
ambapo nyavu za nailoni 310 zilikamatwa, mikuki 20 pamoja na mitumbwi 11.
Alivitaja vifaa vingine
vilivyokamatwa katika operesheni hiyo kuwa ni pamoja na dau moja, kilo
320 za samaki waliovuliwa kwa baruti, nyama ya kasa kilo 65, baruti 17, vibati
14,tmt 22 pamoja na chupa 9 zenye mbolea ya chumvi chumvi zinazotumika kukuzia
milipuko .
Alisema pia walifanikiwa
kukamata kasa wawili, nyavu 18 za kuvulia samaki aina ya kasa pamoja na
kukamata wavuvi sita waliojihusisha na matumizi yasiyo endelevu kwa
rasilimali na kwamba walifikishwa mahakamani huku kasa wawili waliokamatwa
wakiwa nyavuni walirudishwa baharini.
Hata hivyo Ngowo
alieleza kuwa katika utendaji kazi wao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
mbalimbali kwani idadi kubwa ya jamii inayoishi ndani mwa hifadhi wamekuwa
wakitegemea zaidi rasilimali za bahari kuendesha maisha yao licha ya wao kuiwezesha
kwa kiasi kidogo hivyo wao kushindwa kuwaanzishia wote miradi mbadala.
Kwa mujibu wa Ngowo aliiomba wiraza kuwapelekea wataalamu wa
mienendo ya na tabia ya bahari (oceangrapy) kutambua chanzo halisi cha kumeguka
kwa kipande cha ardhi ya pwani ili waweze kufanya utafiti na
kushauri nini kifanyike licha ya kuwa zinafanyika jitihada za kufukiwa ikiwa ni
pamoja na wizara ama makampuni yanayonufaika na uvunaji wa gesi kuchangia kiasi
fulani kama mchango wao ili kusaidia katika uendeshaji wa shughuli kama sehemu
ya mchango katika uhifadhi.
“Naibu waziri tunaomba
tusaidiwe wataalamu wa mienendo ya bahari na tabia ili kutambua chanzo halisi
cha kumeguka kwa kipande cha ardhi ya pwani ili kushauri nini kifanyike ikiwa
ni pamoja na kufanya mazungumzo na wizara au makampuni ambayo yananufaika na
uvunaji wa gesi ili kuchangia kiasi cha fedha kama sehemu yao yamchango katika
uendeshaji na ikizingatiwa visima vyote vipo ndani ya bahari”.Alisema Ngowo.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD