TANGAZO
WAZIRI WA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO FENELLA MUKANGARA WAKATI ANAFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAOFISA MAWASILIANO SERIKALINI KWENYE UKUMBI WA NAF.
Na Clarence Chilumba, Mtwara.
Wanasiasa hapa nchini wameaswa kuacha utamaduni wa kusambaza taarifa zisizo na tija kwa vijana ili wasijitokeze kuipigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa kwani kwa kufanya hivyo kutasababisha nchi kuingia kwenye mgogoro usio na maana kwa ustawi wa Taifa.
Pia vijana nao wametakiwa kutoshabikia kauli na matamshi ya baadhi ya wanasiasa yasiyo na busara ambayo kwa sasa hayana nafasi hapa nchini hasa kuelekea kwenye mchakato wa kupata katiba mpya itakayoongoza nchi.
Hayo yalisemwa jana na waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt.Fenella Mukangara wakati akifungua kikao kazi cha maafisa mawasiliano serikalini kikao kilichowashirikisha pia wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini kwenye ikumbi wa Naf manispaa ya Mtwara Mikindani.
Alisema maofisa mawasiliano serikalini wana kazi ya kutoa taarifa muhimu za serikali kwa vyombo vya habari sambamba na kuangalia na kuimarisha utendaji kazi kwenye taasisi na Halmashauri wanazofanyia kazi.
“Mkutano huu unafanyika kipindi ambacho tunaelekea katika zoezi muhimu la kuipigia kura katiba inayopendekezwa …pia tuna uchaguzi mkuu mbele yetu na nyinyi kwa taaluma zenu za mawasiliano mna jukumu kubwa la kuwawezesha watanzania kuielewa katiba inayopendekezwa na hatimaye kushiriki katika kuipigia kura”.Alisema Mukangara.
Kwa mujibu wa waziri huyo alisema kuwa wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini wana wajibu wa kuhakikisha kuwa wananchi wanaelimishwa kuhusu umuhimu wa kujitokeza kuipigia kura ya ndio katiba inayopendekezwa muda utakapofika.
Alisema kupitia mafunzo hayo ya siku saba maofisa mawasiliano serikalini watapata ufahamu na kuwa chachu ya kuboresha shughuli za mawasiliano serikalini na kuongeza ufanisi katika kuelimisha jamii.
Mwisho.
Katibu mkuu wizara ya Habari,vijana,utamaduni na michezo
Katibu mkuu idara ya Habari maelezo Assay Mwambene wakati akiongea kwenye kikao kazi cha maofisa mawasiliano serikalini
Waziri Fenella Mukangara akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini
Baadhi ya maofisa mawasiliano serikalini wakifuatilia mkutano huo
Maofisa mawasiliano serikalini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa habari,vijana,utamaduni na michezo
Mwenyekiti wa muda wa chama cha maofisa mawasiliano serikalini (TAGCO) Inocent Mungy akibadilishana mawazo na Nevile Meena
Wahariri wa vyombo vya habari wakifuatilia mkutano wa maofisa mawasiliano serikalini
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD