TANGAZO
MWENYEKITI WA KAMATI NDOGO YA BUNGE YA KILIMO,MAJI NA MIFUGO AMINA MAKILAGI AKITOA MAELEKEZO KWA MKURUGENZI WA MANAWASA INJINIA NUNTUFYE DAVID WAKATI WA ZIARA YA KAMATI HIYO.
Na Clarence Chilumba,Masasi.
Kamati ndogo ya kudumu ya bunge la jamhuri ya muungano
wa Tanzania ya kilimo, maji na mifugo imeipongeza mamlaka ya maji safi na usafi
wa mazingira Masasi-Nachingwea (Manawasa) kwa namna inavyofanya kazi katika
kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa wilaya za Masasi na Nachingwea mkoani
Lindi.
Aidha kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa
miradi ya maji katika mikoa ya Lindi, Mtwara pamoja na Pwani tofauti na maeneo
mengine waliyowahi kufika na kwamba hizo zote ni jitihada zinazofanywa na
serikali katika kuhakikisha kuwa kila mwananchi wa mjini na yule wa kijijini
wanapata huduma ya maji safi na salama.
Pia kamati ya maji,kilimo na mifugo imeipongeza
serikali katika utekelezaji wake wa miradi ya maendeleo ambayo kwa sasa inatoa
picha halisi ya kazi kubwa inayofanywa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto
zinazochangia kuzorotesha miradi hiyo ikiwemo ucheleweshwaji wa fedha.
Hayo yalibainishwa na mwenyekiti wa kamati ndogo ya
kudumu ya bunge ya kilimo,maji na mifugo Amina Makilagi wakati wa ziara ya
kamati hiyo mjini Masasi iliyokuwa na lengo la kukagua miradi mbalimbali ya
maji ikiwemo mradi mkubwa wa maji wa Mbwinji unaotoa huduma katika wilaya mbili
za Nachingwea na Masasi.
Alisema lengo la serikali ni kuonha kwamba watanzania
wote wananfadi matunda ya nchi yao katika kupata huduma bora na kwamba lengo
lilikuwa ni kutoa huduma ya maji kwa wananchi kufikia asilimia 85 kwa wakazi wa mijini na asilimia
65 kwa wananchi waishio vijiijini kitu ambacho katika ziara yao wamejionea
wenyewe namna miradi hiyo inavyotoa huduma.
Makilagi alisema tatizo lililopo kwa sasa linalochangia
kuzorota ama kutofanyika kabisa kwa miradi ya maendeleo hasa ile ya maji,kilimo
na mifugo ni mtiririko mdogo wa fedha kutoka serikalini na kwamba wameiomba
serikali kuhakikisha kuwa inapeleka fedha za miradi ya maendeleo kwa wakati.
Mwisho.
INJINIA NUNTUFYE DAVID AKITOA MAELEZO MBELE YA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO KWENYE ENEO LA CHANZO CHA MAJI HAYO
MKURUGENZI WA MANAWASA NUNTUFYE DAVID AKIWAONESHA WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA KILIMO,MAJI NA MIFUGO NAMNA SHUGHULI ZA MAJI ZINAVYOFANYIKA.
WAJUMBE WA KAMATI NDOGO YA BUNGE WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA BODI YA MANAWASA
"MANAWASA TUKO KIKAZI ZAIDI" NDIVYO ANAVYOSEMA INJINIA NUNTUFYE DAVID KWA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO AMINA MAKILAGI.
MJUMBE WA KAMATI HIYO ASAA HAMADI AKIPANDA NGAZI KWENYE TANKI LA MAJI LENYE UWEZO WA KUHIFADHI MAJI LITA MILIONI 4 KATIKA ENEO LA MIGONGO MJINI MASASI.
MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO,MIFUGO NA MAJI AMINA MAKILAGI NAYE AKIPANDA TANKI LA MAJI KWA LENGO LA KUJIONEA SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA MANAWASA.
WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE WAKIANGALIA ENEO AMBALO MAJI HAYO YA MBWINJI HUFIKIA YANAPOTOKA KWENYE CHANZO CHA MAJI NA HAPA NI KATIKA ENEO LA MAILI SITA.
"TUTAHAKIKISHA WANANCHI WA MJI WA MASASI NA NACHINGWEA WANAPATA MAJI SAFI NA SALAMA KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU."(NUNTUFYE DAVID)
HAPA NDIPO MAJI YANAPOCHUJWA BAADA YA KUTOKA KWENYE VYANZO VYA MAJI KATIKA ENEO LA MBWINJI
MWENYEKITI WA BODI YA MANAWASA MATERNUS MALIBICHE AKIONGOZA KIKAO NA KAMATI HIYO YA BUNGE KWENYE UKUMBI WA OFISI ZA MAMLAKA HIYO ULIOPO MJINI MASASI.
"TAZAMENI UBORA WA MATANKI YETU YA KUHIFADHIA MAJI" (INJINIA NUNTUFYE DAVID-MKURUGENZI WA MANAWASA)
MASHINE ZA KUCHAKATA MAJI ZILIZOPO KWENYE ENEO LA MAILI SITA MJINI MASASI
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD