TANGAZO
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Wanaume hapa nchini
wameaswa kujitokeza kuhudhuria mafunzo mbalimbali ya ujasiliamali ambayo
yamekuwa yakitolewa na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali yenye lengo la
kuwaadaa watanzania kuwa wajasiliamali ili kupunguza umasikini.
Pia wametakiwa kuondoa
dhana kuwa mafunzo hayo huandaliwa kwa ajili ya wanawake pekee kitu ambacho si
kweli kwani mafunzo hayo huandaliwa kwa watu wote bila kujali jinsia zao.
Hayo yalisemwa jana na
mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Isagnel creating and
Blowssoms mchungaji Israel Ernest wa kanisa la Acole Ministry la jijini Dar es
salaam wakati wa mafunzo ya siku tatu ya wajasiliamali mjini hapa.
Alisema taasisi yake
imekuwa ikitoa mafunzo hayo kwa muda mrefu sasa kwenye mikoa yote hapa nchini
na kwamba lengo lao ni kuwafikia watanzania wote ili waweze kupata elimu ya ujasiliamali
na kuachana na dhana ya kusubiri ajira kutoka serikalini.
Alisema kinachochangia
umasikini hapa nchini ni dhana iliyojengeka kwa wananchi wengi hasa vijana
wanaohitimu vyuo vikuu kudhani kuwa njia pekee ya wao kupata ajira ni kwa
kuajiriwa na serikali mazingira ambayo husababisha kundi hilo kubwa kubaki
vijiweni bila shughuli zozote za uzalishaji mali.
Mchungaji huyo alisema
katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika kwenye ukumbi wa kanisa katoliki
Masasi yalijumuisha wajasiliamali 120 kutoka wilaya za Newala, Tandahimba,
Nanyumbu na Masasi mkoani Mtwara pamoja na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
ambapo kwa mara ya kwanza wanaume nao walijitokeza.
Kwa mujibu wa mchungaji
Israel alisema wamefanikiwa kufundisha wajasiliamali hao jumla ya masomo 15
yakiwemo yale ya utengenezaji wa bidhaa za viwandani na ufugaji kama vile
batiki,vikoi,siagi,unga wa karanga sabuni za maji na mche,rangi za majumbani,mafuta
ya kupikia na kupaka pamoja na namna ya utengenezaji wa mashine za uanguaji wa
vifaranga.
“Taasisi yetu kwa sasa
ni kongwe kwa kuwa tumefanikiwa kuwafikia watanzania karibu mikoa yote ya
Tanzania bara na hata ile ya Zanzibar na kwamba hadi sasa ni mikoa mitatu pekee
ya Kigoma,Lindi na Iringa ndiyo ambayo hatujawafikia kuwapa elimu hii na kwamba
kwa mwaka huu tumejipanga kuwafikia mapema iwezekanavyo”.Alisema.
Alizitaja changamoto
kadhaa wanazokumbana nazo ikiwa ni pamoja na wakati mwingine kupokea wanafunzi
ambao hawajui kusoma na kuandika hivyo kuwapa shida katika masomo yao ya
nadharia na kwamba ili kuwasaidia wamekuwa wakijitahidi kuwafiundisha zaidi kwa
kutumia vitendo na wengi wao wamefanikiwa.
Aidha changamoto
nyingine ni kupokea wanafunzi wenye ulemavu wa macho lakini kwa kutumia mbinu
mbadala wamekuwa wakifanikiwa kuwafikishia ujumbe wao kwao huku kubwa zaidi ni
kwa wanaume kutojitokeza kuhudhuria mafunzo ya ujasiliamali kwa madai kuwa yapo
kwa ajili ya wanawake pekee.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD