TANGAZO
Na Clarence Chilumba, Ruangwa
Zaidi
ya watu 2500 wilayani Ruangwa mkoani
Lindi wamepata huduma ya kupima macho, kisukari,shinikizo la
damu na wangine 144 wamefanyiwa operesheni ya macho baada ya mbunge
wa jimbo hilo Kasimu Majaliwa kwa kushirikiana na taasisi ya
Bilal muslim kutoa huduma hiyo bure kwa wananchi wa jimbo hilo na
maeneo ya jirani.
Hayo yalibainishwa na mratibu msaidizi wa
taasisi ya Bilal Muslim Nurdini Ali wakati alipokuwa anazungumza na
waandishi wa habari waliotembelea kwenye zoezi hilo lilofanyika kwa
muda wa siku tatu kwenye uwanja wa shule ya msingi Ruangwa.
Nurdin alisema kuwa mwaka huu wananchi
wamejitokeza kwa wingi ukilinganisha na idadi ya mwaka 2012
wakati wanaendesha zoezi hilo watu waliopata huduma za kupima
macho na kupata dawa pamoja na miwani na upasuaji ilikuwa
ndogo.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa
wilaya hiyo Tanasia Ndaka alisema kutolewa kwa huduma hiyo
bure katika maeneo yao kumewasaidia wananchi wenye kipato kidogo
wasio kuwa na uwezo kusafiri kutafuta huduma hiyo.
“Unajua huduma iliyotolewa ni kubwa kwani
kwa kipato cha wananchi wa kijijini kama mimi siwezi kujigharamia hivyo
tuna kila sababu ya kutoa shukrani za dhati kwa mbunge wetu Kasimu Majaliwa
aliyefanikisha kutuletea huduma hii”. Alisema.
Kwa pande wake mbunge wa jimbo la Ruangwa kasimu Majaliwa
alisema lengo la zoezi hilo ni kuboresha afya kwa wananchi wa jimbo
hilo ili waweze kuendelea kuongeza mapato yao binafsi na Halmashauri kwa ujumla
ili kutekeleza azma ya matokeo makubwa sasa (BRN).
Majaliwa alisema ili kuhakikisha na kutekeleza
mpango huo wa matokeo makubwa sasa katika Halmashauri hiyo kwenye
sekta ya afya tayari wameanza zoezi la kuboresha miundombinu ya Hospitali kwa
kuongeza majengo na kununua mashine ya upasuaji mkubwa ambayo ina
uwezo wa kufanya kazi masaa 24 sambamba na kuwa na madaktari bingwa 26 wa
magonjwa mbalimbali.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD