TANGAZO
Na Hamisi Nasiri, Liwale
Mjumbe wa mkutano mkuu taifa chama cha wananchi CUF Zuberi Kuchauka ametangaza nia ya kuwania ubunge jimbo la Liwale huku akimuonya mbunge wa jimbo hilo afanye siasa badala ya vitendo vinavyokiuka haki za binaadamu.
Kuchauka alitangaza nia hiyo kwenye mkutano wa
hadhari wa kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa
kukichagua chama cha hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika
mwezi uliopita
“Nimetafakari kufuatia maelezo ya chama changu,
nimejipima na nimetazama hali halisi ya maendeleo na kero ya za huduma mbovu za
muda mrefu kwa wananchi jambo ambalo kwa bahati mbaya jimbo hilo linaongozwa na
viongozi wa ccm tangu uhuru”.Alisema.
Kufuatia mabadiliko ya CUF na UKAWA tumejipanga kuchukua dola
mwaka huu ,basi nimefikia uamuzi wa kugombea ubunge Liwale nimesukumwa na
umasikini wa wananchi ,huduma zote za jamii ni mbovu ,huvyo nimedhamiria kuleta
mabadilikona siwezi kumuunga mkono eti ni ndugu yangu alisema Kuchauka.
Alisema umasikini wa jimbo kama ulivyo kwa watanzania wengi nchini
,chanzo chake ni sera na mipango mibovu ya CCM ,ingawa lina rasilimali nyingi
kama Ardhi ,misitu ,lakini sababu ya mipango ya sera mbovu wananchi
wanaishia kunyonywa .
Kuchauka alisema Jambo la kwanza akishinda nafasi hiyo endapo
atapitishwa na chama chake, ataweka mipango ambayo itawasaidia wananchi
waondokane na umasikini na ndio ugomvi uliopo hapa nchini na atapambana na wizi
wa fedha za kodi za wananchi za miradi ya maendeleo kama barabara, maji, ujenzi
wa zahanati na vituo vya afya zinazoishiwa kuliwa na watendaji wa halmashauri,
Taasisi za umma na serikali kuu kuhakikisha zinafanya kazi zilizolengwa.
“Nitapambana na wizi wa fedha ili miradi ilenge kufanya kazi
iliyokusudiwa kama ilivyopangwa na njia nitakayotumia ni kuweka mipango mizuri
na usimamizi” alisema kuchauka
Alisema kuwa atasimamia suala la elimu kwa kuhakikisha kuwa
kila mtoto anayestaili kwenda shule anakwenda na waliochaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza wanaripoti shuleni.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD