TANGAZO
WANANE KIZIMBANI KWA MAUAJI YA MLINZI WA OFISI YA CHAMA CHA MSINGI-CHIKUNDI
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Wakazi wanane wa kijiji
cha Mtunungu kata ya mwena Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara
wamepandishwa kizimbani kujibu shitaka linalowakabili la mauaji ya mlinzi wa
gahala la chama cha msingi Chikundi Amcoss Valentino Gilbert (70) mkazi wa
kijiji cha Chikundi wilayani Masasi.
Watuhumiwa waliofikishwa
mahakamani hapo jana kujibu shitaka hilo ni Hassani Chimkambi,Philipo
Kambanga,Ismaili Chilumba pamoja na Bakari Ibrahimu wote wakiwa ni wakazi wa
kijiji cha Mtunungu wilayani Masasi.
Wengine waliopandishwa
kizimbani ni Ismaili Bakari,Mpandula Mohamedi,Thabiti Mkwavila pamoja na Nicholaus
Liumbo ambao walifikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya
wilaya ya Masasi Asha Mwetindwa na
kusomewa shitaka na mwendesha mashtaka Iddi Omari.
Iddi alidai kuwa
watuhumiwa hao walitenda kosa hilo la mauaji ya kukusudia mnamo Desemba 30,
mwaka jana majira ya saa 8:30 usiku katika
eneo la ofisi za chama cha msingi Chikundi kijiji cha Mtunungu wilayani humo huku
wakijua kuwa ni kosa la jinai chini ya kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu
sura ya 16.
Alidai kuwa watuhumiwa
hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya
kusikiliza kesi hiyo na kwamba kwa sasa iko kwenye hatua za awali za uchunguzi
na uchunguzi huo utakapokamilika kesi hiyo itahamishiwa mahakama ya mkoa
Mtwara.
Watuhumiwa hao walirudishwa
rumande baada ya kukosa dhamana na kwamba kesi hiyo itatajwa tena mnamo Januari
19 mwaka huu mahakama ya wilaya ya Masasi.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD