TANGAZO
BAADHI YA WANACHAMA WA TALGWU MKOANI MTWARA WAKIWA KWENYE MKUTANO NA VIONGOZI WA CHAMA HICHO TAIFA.
Na Clarence Chilumba,
Mtwara.
Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa hapa nchini
TALGWU kimesema hakitashiriki uchaguzi mkuu wa serikali wa kumchagua Raisi,
wabunge na madiwani unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu endapo
serikali haitolipa madeni sugu ya wafanyakazi hapa nchini.
Aidha taarifa hiyo imedai kuwa tangu kuanzishwa kwa
chama hicho serikali imekuwa ikisuasua kulipa deni la shilingi billioni 17
jambo linaloonesha kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania wameshindwa
kuthamini mchango wa wafanyakazi wake huku wakifanya kazi katika mazingira
magumu.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na naibu katibu
mkuu wa chama hicho Njaa Kibwana wakati anaongea na wanachama wa chama hicho katika
Halmashauri ya manispaa ya Mtwara wakati wa ziara yake mkoani humo.
Alisema serikali inapaswa kutambua mchango unaotolewa
na wafanyakazi wa sekta zote hapa nchini na kwamba wakati wa kuendelea
kunyanyaswa umeisha na badala yake serikali ione umuhimu wa kundi hilo muhimu
kwa kulipa madeni sugu ili kuondoa migogoro isiyo ya lazima.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TALGWU mkoa wa Mtwara
Damalesi Mwendo aliwaasa viongozi wa chama hicho Taifa kujali wanachama wake
kwa kuhakikisha wale wote waliojaza fomu za mikopo wanapatiwa pasipo usumbufu
wowote.
Viongozi wa chama cha wafanyakazi Taifa TALGWU wapo ziarani mkoani Mtwara kwa lengo la
kuwakumbusha wanachama wake majukumu ya
chama hicho pamoja na faida zikiwemo
changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wa majukumu yao.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD