MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA RUANGWA MKOANI LINDI WAKIFUATILIA MKUTANO WA KUPITISHA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA WA 2015/2016 KATIKA UKUMBI WA RUTESCO WILAYANI HUMO.
Na Clarence Chilumba, Ruangwa.
Baraza
la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kwa kauli moja limepitisha
bajeti ya zaidi ya Shilingi Bilioni 20 zitakazokusanywa na kuelekezwa katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye kata, vijiji na mitaa ya
halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Kati
ya kiasi hicho cha fedha Shilingi Bilioni 1,627,449,600 inatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo
vyake mbalimbali vya mapato ya ndani ambapo ruzuku kutoka Serikali
kuu pamoja na misaada kutoka kwa wafadhili ikitarajiwa kuwa ni zaidi ya
shilingi bilioni 4,885,000,916.
Akisoma
taarifa ya mapendekezo ya mpango wa
maendeleo na bajeti ya Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa mwaka wa fedha
2015/2016 katika mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri hiyo mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Reuben Mfune alisema makadirio ya
bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016
ni Shilingi Bilioni 20,361,371,116.
Alisema
makadirio hayo yamepanda kutoka shilingi
Bilioni 15,279,186,916 kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 ingawa hadi kufikia
novemba 2014 Halmashauri hiyo ilifanikiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 5,657,995,774 kutokana na vyanzo
vyake vya ndani sawa na asilimia 34 ya makadirio yake.
Kwa
mujibu wa Mfune alisema kuwa Halmashauri inatarajia kutumia shilingi Bilioni
4,885,000,916 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia
vyanzo vya mapato kama vile ruzuku
kutoka serikali kuu, vyanzo vya ndani pamoja na fedha kutoka kwenye programu za
Elimu sekondari (SEDP), maji na usafi (NWSSP) pamoja na mfuko wa barabara.
Alisema
licha ya kupitisha makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2015/2016 Halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali
ambazo huathiri utekelezaji wa malengo ya utekelezaji yanayowekwa kama vile
kucheleweshwa kwa fedha za ruzuku kutoka serikali kuu, pamoja na kutofikiwa kwa malengo ya ukusanyaji
mapato kwenye baadhi ya vyanzo vya Halmashauri.
Alizitaja
changamoto zingine kuwa ni upungufu wa
watumishi wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ngazi
ya chini wakiwemo maofisa watendaji wa kata na vijiji, mwitikio mdogo wa
wananchi katika kuchangia fedha na kushiriki kwa nguvu zao pamoja na miundo
mbinu duni ya barabara na mawasiliano.
“Watendaji
wenzangu leo kwa kauli moja madiwani wamepitisha bajeti ya Halmashauri yetu ya
Ruangwa…huu ni mwanzo tu wa kazi kubwa iliyopo mbele yetu ya kuibua na
kusimamia miradi yote ya maendeleo iliyobaki na ile inayotarajiwa kutekelezwa
kwa mwaka huu wa fedha”.Alisema Mfune.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Ruangwa Issa Libaba aliwataka
watendaji wa Halmashauri hiyo kuwa na uwazi kwenye mapokezi ya fedha za miradi
kutoka serikali kuu pamoja na misaada ya wahisani sambamba na ushirikiano baina
ya watendaji na madiwani ili kufikia malengo mbalimbali yaliyowekwa.
Alisema
ni vyema watendaji hao wakatumia muda mwingi katika kuitekeleza bajeti hiyo
iliyopitishwa kwa vitendo na kwamba watambue kwamba serikali imewapa madaraka
ili wawatumikie wananchi wa wilaya hiyo.
Mwisho.
|