TANGAZO
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANDREW MTUMUSHA
Na Clarence Chilumba, Masasi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi ambaye pia ni
diwani wa kata ya Nyasa Andrew Mtumusha ametoa onyo kali kwa watendaji wa
kata,mtaa wenye tabia ya kudai malipo kutoka kwa vikundi vya wajasiliamali
wajane pale vikundi hivyo vinapohitaji huduma ikiwemo ya kupitishiwa mihtasari
yao ya benki.
Aidha ameweka wazi msimamo wake kwa viongozi hao kuwa
atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo vinavyokwenda kinyume na maadili ya
utumsihi wa umma basi atosita kumchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja
na kumsimamisha kazi na kumburuza mahakamani.
Alitoa kauli hiyo jana mjini humo wakati anafungua mafunzo
ya siku moja ya ya kamati za usimamizi wa miradi ya Tasaf katika ukumbi wa
kituo cha walimu mkomaindo ambapo alisema watendaji hao wamekuwa kero na kikwazo
kikubwa kwa wananchi pale wanapohitaji huduma kutoka kwao.
Alisema miradi mbalimbali imekuwa ikiletwa na serikali ili
kuinua kipato cha wananchi wake lakini makundi hayo maalumu yamekuwa
yakikumbana na changamoto kubwa kutoka kwa watendaji hao ambao kwenye maeneo
yao ya kazi wamejigeuza kuwa miungu watu.
“Naagiza kwa watendaji wote wa kata,mitaa Halmashauri ya mji
wa Masasi kuwa hakuna kiongzoi yeyeote wa ngazi hiyo aliyepewa mamalak ya
kuwalipisha ushuru wowote wajane waliopatiwa na wale watakaopatiwa mikopo ya
wajasiliamali na kwamba kufanya hivyo ni kosa na nitawashitaki”.Alisema
Mtumusha.
Alisema mara nyingi amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa
baadhi ya viongozi wa vikundi hivyo kuwa wamekuwa wakiwatoza ushuru na
watendaji hao pindi wanapokwenda kupitisha mihtasari yao na kwamba wanapaswa
kutambua kuwa serikali imewapa nafasi hizo ili watoe huduma kwa wananchi na si
vinginevyo.
Mtumusha alisema watendaji kama hao hawapaswi kuachwa
wakiendelea kufanya kazi ndani ya Halmashauri ya mji na kwamba endapo watafanya
kazi kana kwamba wao ni miungu watu atakula nao sahani moja.
Alisema licha ya vikundi hivyo kulalamika lakini bado hata
wanacnhi wa kawaida wamekuwa wakitoa malalamiko yao kuhusu watendaji hao huku
akiwaasa kuwa wafanye kazi zao kwa kufuata kanuni na sheria za mamlaka ya
serikali za mitaa ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza kati ya wananchi
na Halmashuri yao.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD