TANGAZO
Katibu Tawala wilaya ya Masasi Danford Peter |
Na Clarence Chilumba,
Masasi.
Wananchi wa Halmashauri ya
mji wa Masasi mkoani Mtwara wameaswa kuthamini mchango walioutoa waasisi wa
serikali ya mapinduzi ya Zanzibari waliojitoa kwa ajili ya maslahi ya wananchi
wa Zanzibar katika kuuondoa utawala dhalimu wa kisultani ambao haukuwahi
kuthamini maisha ya wazanzibari.
Aidha wametakiwa
kudumisha umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa watanzania na kwamba amani
iliyopo kwa sasa na wanayoifurahia ni mafanikio makubwa ya viongozi waasisi wa
serikali ya mapinduzi ya zanzibari pamoja na ile ya Tanganyika.
Pia wamekumbushwa
kutumia siku hiyo muhimu kwa Wanzazibari kama sehemu ya kufanya maombi ya
kuliombea Taifa la Tanzania hasa katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka
huu ili uende kwa amani na usalama sambamba na kupata viongozi bora na walio
waadilifu.
Hayo yalisemwa leo na katibu
tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kwa niaba ya mkuu wa
wilaya ya Masasi Danford Peter wakati akiwahutubia maelfu ya wananchi wa kata
ya Chanikanguo Halmashauri ya mji wa Masasi waliojitokeza katika kumbukumbu ya
maadhimisho ya miaka 51 ya mapinduzi ya Zanzibari.
Alisema wengi wa vijana
wa sasa hawajui maana na hata umuhimu wa mapinduzi ya Zanzibari na kwamba ili
kufahamu wanapaswa kusoma vitabu vinavyoelezea historia ya mapinduzi hayo ambapo
watajua harakati zilizofanywa na kundi la vijana 17 wanaharakati wa wakati huo
visiwani Zanzibari wakiongozwa na hayati Sheikh Abeid Amani Karume.
Katibu tawala huyo
alisema tukio hilo la kufanya mabadiliko ya mfumo wa utawala kutoka kwa
watawala wachache mnamo Januari 12, 1967 na kuleta madaraka kwa wengi kwa
maslahi ya wananchi ndicho kitu kinachowafanya watanzania bila kujali itikadi
zao za kisiasa,dini au rangi kuungana na wananchi wa Zanzibari katika
kuadhimisha maadhimisho hayo.
Alisema katika
kuadhimisha siku hiyo watanzania wanapaswa kuzingatia elimu ya watoto
waliofikia umri wa kwenda shule pamoja na wale waliochaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza na kwamba hilo si ombi bali ni amri ambayo iko kisheria na kwamba
kila mzazi kwa nafasi yake anapaswa kutimiza wajibu wake.
Kwa mujibu wa Danford
alisema suala la elimu ni muhimu kwa kila Mtanzania kwani ni chombo pekee
kinachomkomboa mtu ili aweze kukabiliana na mazingira yanayomzunguka katika
jamii ambapo amewaonya wazazi ambao watakiuka agizo hillo halali la serikali.
Alisema ili kuyaenzi
mapinduzi ya Zanzibari wananchi wanapaswa kutumia vizuri mvua zinazoendelea
kunyesha hivi sasa mkoani humo ili waweze kujitosheleza kwa chakula na kwamba
kwa kufanya hivyo watakabiliana na baa la njaa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD